Pre GE2025 Ni vema CHADEMA wasishupaze shingo itavunjika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sijawahi kumuelewa pasikali bora mwasambwa anaeleweka mchumia tumboo..
 
hatuichagui ila alichosema nape ndo ukweli wenyewe ccm haiongozi nchi kuchaguliwa bali kwa sababu wao wanaandaa uchaguzi kisha wanajitangaza kuwa wameshinda tunahitaji mabadiliko.
Ni kweli chadema haijajipanga vyema kuing'oa ccm madarakani lakini ni bora chadema kuliko ccm
 
Ushauri mbovu na wa hovyo...

Yote yanapaswa kufanyika kwa wakati mmoja; kushiriki uchaguzi na kudai katiba mpya...

Ni kweli mazingira na uwanja wa uchaguzi si fair na siyo sawa kwa vyama vya siasa shiriki vyote...

Mazingira na dalili zote zinaonesha kuwa CCM, chama kinachoongoza serikali sasa na ambacho makada wake licha ya kwamba ni washiriki wa uchaguzi, pia ndio watunga kanuni na ni marefa/waamuzi wa uchaguzi wote...

Pamoja na mazingira haya magumu, lazima tupambane nao ndani ya mazingira hayahaya kwa kutumia njia zote halali ikiwemo mahakama hata kama haiaminiki kwa 100%....

Ndiyo maana kuna kesi inaendelea kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi huu. Au hujui...?

HAKUNA KUSUSA. NI KUPAMBANA NAO HADI KIELEWEKE....!!
 
Ni kweli chadema haijajipanga vyema kuing'oa ccm madarakani lakini ni bora chadema kuliko ccm
Utawasaidia sana wapiga kura ukiusema huo ubora wa Chadema, ili wapiga kura tuwachague Chadema tuwakabidhi Ikulu yetu.
P
 
Njaa na mapambano haviendi pamoja.

Chadema wana njaa na wakati huo huo wanatakiwa kupambana. Unadhani inawezekana kususia uchaguzi?
 
CHADEMA ni nini au ni nani?

Siyo itikadi na imani ya wafuasi?
Siyo watu ambao na wao wanatakiwa kula, kusomesha na kuishi leo?
Siyo mimi na wewe?

Waache siasa ili wafanye nini? Wakiacha kwa ajili ya mabadiliko ya baadaye je leo itakuwaje?

Lazima tuishi leo, sasa, tuendelee kudai tume huru, katiba, lakini tuendelee kuminyana vikali na ccm leo na sasa na hata milele.

Ebooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…