Pre GE2025 Ni vema majimbo ya Kawe, Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanywe kutokana na Wingi wa Wananchi na Huduma za kiuchumi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa logic yako, ni wazi kwamba majimbo mengi sana yatakua na huitaji huo kwa kugawanywa......mfano Nyamagana n.k Mm naamini majimbo mengi ya mijini hayastahili kugawanywa hata kama yana watu wengi sana, kwasababu mbunge wake ana urahisi wa kuwafikia na kuwahudumia wapiga kura wake kuliko majimbo yasiyo ya mijini ambayo kijografia hua ni makubwa sana na miundombinu yake huwa duni.
 
Hesabu zako hspa ni kuwafanyia wepesi Lema,Sugu na B Halima. Na bila shaka nawe ni Mbunge.
 
yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu hoja hii aliisema sana tena kisayansi sayansi ya siasa kuhusu uwakilishi wa watu:

Tundu Lissu asisitiza Mabonde, milima hayapigi kura bali ni watu na kuwa kura moja ya Dar es Salaam iwe sawa na kura moja Bukoba, Mbeya n.k na kurejea takwimu za Tume ya Uchaguzi :

bali watu Mtwara wapiga kura 930,000 majimba bunge 10, huku Dar es Salaam watu 3,000,000 majimbo 10, Mbeya 1,000,000 majimbo 7.

Majimbo-bunge lazima yawe na idadi sawa ya wapiga kura ili kura zote ziwe na uzito unaolingana. Mfawanyo wa maeneo / jimbo bunge lazima yawe na idadi sawa

Kutoka maktaba :

SENSA NA DEMOKRASIA
Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi
Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.

Source : Hii ndiyo tofauti ya Sensa ya 2022 na zilizopita
 

12 April 2024

TUNDU LISSU - TUME HURU YA UCHAGUZI SIYO HURU, RAIS ANATEUA NA KUTENGUA WAJUMBE WAKATI PIA NI MGOMBEA KTK UCHAGUZI

View: https://m.youtube.com/watch?v=gbl_dbYBof0
Toka maktaba :
6 August 2022

Tundu Lissu: Idadi ya wabunge wa kuchaguliwa iwiane na idadi ya raia wanaowakilisha​


Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media
Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha ... Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema..... soma zaidi : source : Hotuba ya Jaji Josefu Warioba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Tanzania
 
UGAWAJI WA MAJIMBO KWA MINAJILI YA KUJIHAKIKISHIA KURA

Mwanahistoria nguli Mohamed Said wa JamiiForums anatukumbusha - ''Zanzibar chini ya utawala Waingereza hapakuwa na wizi wa kura. ASP walikuwa wanashindwa kupitia gerrymandering. Huu ni ujanja katika kukata majimbo ya uchaguzi. gerund or present participle: gerrymandering manipulate the boundaries of (an electoral constituency) so as to favour one party or class "


Ramani ikionesha mikoa mipya ya Simiyu, Geita, Katavi, Njombe, Songwe na ule mpya unaopigiwa chapuo mkoa wa Chato uanzishwe.

Picha maktaba: mfano kuonesha michezo ya kugawa majimbo kwa kuangalia CCM ijikusanyie wabunge wengi kupitia idadi kubwa ya majimbo bunge yenye idadi ndogo ya wapiga kura.




Ni kweli kwa ajili ya kupeleka huduma karibu na wananchi au ni kwa ajili ya kujiongezea viti vya ubunge na nafasi zingine za kuendelea kutawala?



Gerrymandering ni kutengeneza mipaka ya majimbo bunge mengi lengo ili kuhakikishia kupata wabunge wengi na kushinda uchaguzi.

Gerrymandering is to manipulate district boundaries, for political advantage.

gerrymandering
  1. manipulate the boundaries of (an electoral constituency) so as to favour one party or class.
    • achieve (a result) by gerrymandering.
      "an attempt to gerrymander the election result
 
Mawazo ya kipuuzi kamahaya ndio yanafanya hiinchi kuendelea kuwa ombaomba.

Niulafi wakugawana koditu hakuna faida yoyote.
 
Tunajua lengo lako uwaokoe Tulia, Gambo na Mfufuwa wafu. Hakuna namna lazima wachezee kichapo
 
Hili ni wazo la ki-ndezi kabisa. Na nyinyi ndiyo maadui wa maendeleo yetu. Sijui umetumia vigezo gani kuja na hoja hiyo.

Sioni sababu ya kugawanya Mbeya. Lakini wote wanaokuja na hoja ya kuigawanya Mbeya wanataka kumuokoa Tulia Ackson dhidi ya Sugu. Kwani hata mukigawa hiyo sehemu nyingine mna uhakika gani kama Tulia atashinda.

Tuache mawazo MFU yanayoongeza gharama za serikali bila sababu
 
Michezo michafu ya kuangalia mipaka yenye wanaCCM wengi kisha kuiganyanya katika majimbo mengi huku yale yenye wapinzani wengi kuyatengenezea majimbo machache.

Video hii inafafanua michezo hii inayoitwa gerrymandering mahsusi kujihakikishia wabunge wengi kwa hila:


View: https://m.youtube.com/watch?v=bGLRJ12uqmk
 
Hivi kwenye majimbo wabunge Huwa wanalipi zaidi ya porojo??. Jmn anayeleta maendeleo ni mwananchi mwenyewe Kwa kulipa Kodi serikali inaisimamia Kwa kumpeleka maendeleo mwananchi. Hao wabunge hawana jipya ni asubiri serikali iwe na plan ya kupeleka barabarani Wilaya Fulani ya yeye ajipenyeze hapo kujifanya yeye kaleta
 
We Mzee umekuja kupima upepo hapa jf na mawazo yako ya hovyo.
Badala ya majimbo kuunganishwa ili kupunguza gharama za uendeshaji we unawaza kuyapunguza tena ukubwa?!.
usisahau kuna wakuu wa wilaya wamo humo humo, wakuu wa mikoa...bado tu hawatoshi!
 
Majinmbo yapunguzwe, viti maalumu vifutwe, na vyeo vya ukuu wa wilaya vifutwe. Huku kote Kuna wajinga TU wanakula Kodi za wananchi kwa kigezo cha ukada. Fvck ccm
 
Wananchi wanataka kila wilaya iwe na mbunge mmoja ili kuwapunguzia mzigo wa kugharimia serikali wewe unataka kuwaongezea mzigo, akili za wapi hizo?πŸ•πŸ•πŸ•
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…