Pre GE2025 Ni vema majimbo ya Kawe, Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanywe kutokana na Wingi wa Wananchi na Huduma za kiuchumi!

Pre GE2025 Ni vema majimbo ya Kawe, Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanywe kutokana na Wingi wa Wananchi na Huduma za kiuchumi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Majimbo yakigawanywa maana yake pia idadi ya wabunge itaongezeka.

Swali la kujiuliza, je wabunge wakiongezeka kutaleta maendeleo chanya kwa majimbo husika au ndio tutaongeza idadi ya watu wa kusinzia ktk vikao vya bunge kwa kigezo cha kutuwakilisha huku wakizitafuna mil18 za mishahara pamoja na malupulupu kila mwezi?
Hakuna la maana, viongozi wamejaa mpk ngapi ya mtaa unataka mbunge afike kila kaya? utadhani mbunge ndiyo anakusanya kodi
 
Nyerere hakuwa visionary alijikita kuwaiga wazungu kila kitu.

Wabunge walibidi wasiwepo kabisa maana Mimi sioni faida yao zaidi ya kupiga kelele bungeni.

Ilibidi kila mkoa awepo mbunge mmoja tu.
Ukweli pale hakuna bunge lile ni kusanyiko la shetani kabisa
 
sio wazo baya ila ujanja wako tunaujua..
unataka na mdee apate nafasi. unataka na sugu apate nafasi..unataka na rema apate nafasi.

kama una nia ya kweli ya kiuchumi siombaya ila kama nia ni wanasiasa hapo ni kutumia vibaya mali za uma. na hao watu wa majimbo hawana faida yoyote zaidi ya kupiga makofi na kujitungia sheria za kujinufaisha wao.
 
Baada ya ziara yangu ya kichama kutoka Arusha hadi Mbeya kupitia Babati napendekeza majimbo ya uchaguzi ya Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Kadhalika Jimbo langu la Kawe nimeshaomba muda mrefu tu ligawanywe

Mungu wa mbinguni awabariki Tume Huru ya uchaguzi 🌹
Mbeya alikuwa Sugu ni threat kwa mkubwa
Arusha alikuwa Lema ni threat
Kawe alikuwa Halima ni threat
 
Baada ya ziara yangu ya kichama kutoka Arusha hadi Mbeya kupitia Babati napendekeza majimbo ya uchaguzi ya Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Kadhalika Jimbo langu la Kawe nimeshaomba muda mrefu tu ligawanywe

Mungu wa mbinguni awabariki Tume Huru ya uchaguzi 🌹
Hali hii inahuzunisha Sana, Watu badala ya kufikiria juu ya maslahi mapana zaidi ya nchi pamoja na wananchi wake, wao wako busy Sana kuwazia maslahi yao binafsi kupitia vyama vyao vya siasa. I feel ashamed to be Tanzanian. Mambo haya ya maslahi ya vyama vya siasa na wanasiasa wake yamekuwa yakituvuruga Sana sisi wa-Tanzania, nchi imekuwa haisongi mbele kumaendeleo kutokana na mivurugano ambayo imekuwa ikisababishwa na wanasiasa.
 
Baada ya ziara yangu ya kichama kutoka Arusha hadi Mbeya kupitia Babati napendekeza majimbo ya uchaguzi ya Arusha mjini na Mbeya mjini yagawanye kutokana na wingi wa Wananchi na ukuaji mkubwa wa Huduma za kiuchumi

Kadhalika Jimbo langu la Kawe nimeshaomba muda mrefu tu ligawanywe

Mungu wa mbinguni awabariki Tume Huru ya uchaguzi 🌹
Mapendekezo yako ni muhimu sana,sio tu katika maeneo uloyabainisha yapo maeneo mengine nchini yanaonekana kuhitaji kusogezewa huduma zaid...

hata hivyo, labda tutacheki 2030 ikiwa maeneo hayo yatakua yamekidhi vigezo na sifa za kisheria kugawanywa, mpaka kufikia wakati huo..

kwasasa ni eneo moja tu kati ya hayo ndiyo linakaribia kukidhi sifa na vigezo hivyo vya kugawanywa.

Hata hivyo ni matarajio ya wengi kwamba kabla au wakati huo maeneo yote au baadhi ya hayo zaid yatakua yamekidhi vigezo na masharti hayo ya kikatiba 🐒
 
Mleta mada ulishawai kufika jimbo la mvomero. Baadhi ya maeneo wanalazimika kulala njiani ili wafike siku ya pili makao makuu ya wilaya
 
Mbeya: Jimbo moja la Tulia, lingine la Sugu

Arusha: jimbo moja la Lema lingine kapuni
 
Back
Top Bottom