SoC01 Ni vidogo lakini vinakera, na visipofanyiwa kazi umasikini utabaki palepale

SoC01 Ni vidogo lakini vinakera, na visipofanyiwa kazi umasikini utabaki palepale

Stories of Change - 2021 Competition

Ornate

Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
26
Reaction score
33
Sasa imekuwa kama mtindo wa maisha kwa watanzania wengi, bila kufahamu kuwa wanapoteza pesa na muda mwingi ambao ungetumika katika kujenga jamii.

Baadhi ya watu hasa wa maisha ya kawaida kwa kipindi hiki wameonekana wakifanya sherehe nyingi zisizo za lazima. Nabaki najiuliza nini sababu hasa, Ni zawadi tu au kujitafutia sifa za kwamba "walikula wakasaza"

Sherehe zimekuwa nyingi sana, lakini hakuna sababu ya kufanya sherehe hizo, utakuta mtu anamtoa mtoto imezoeleka kama arobaini ya mtoto lakini kinachotokea ni zaidi ya arobaini, haitoshi mtoto au mtu mzima ametimiza miaka fulani ya kuzaliwa na anaamua kukodi muziki na mda mwingine anakesha kabisa. Inasikitisha kuona pesa zinapotea bure bila kazi ya msingi.

Wanawake wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono mambo haya, Hadi wakajikuta wanaunda makundi mbalimbali ili kuchangiana, huku wengine wakitaka sifa zaidi na waonekane zaidi ya wenzao, wananunua zawadi zenye gharama nyingi ili apate sifa pale atakapotunza.

Lakini pia wengi wao, wanapoona wametunza vya kutosha huku hakuna dalili ya wao kufanya sherehe hivyo wanalazimika kukodi muziki bila sababu ambao unagharimu pesa, lengo ni atunzwe tu, hili ni jqmbo la kuangaliwa mara mbili.

Ni machahe tu lakini yana maana ndani yake, embu tujitafakari, tunasubiri Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania aje atuwezeshe wanawake, wakati mtaji wetu mdogo tulionao tunautumia vibaya?

Vikundi tunavyovianzisha ili kutuzana katika sherehe hizo kwanini tusivitumie kutengeneza biashara ili kuinuana kiuchumi ili kufikia Tanzania ya maendeleo.
 
Upvote 1
Kuna kundi moja la KE ambao mmoja wao aki- conceive, wanakusanyana kutoa pongezi na tuzo !!!
 
Back
Top Bottom