Ni vigumu kwa Mwafrika Dr Tedros Ghebreyesus kuendelea kuongoza WHO, Marekani yaondoa fedha za mchango nyuma ya pazia, yashinikiza Tedros aondolewe

Kwa mantiki hizi hakika hatuwezi endelea kokote. Mbona hoja ya Trump ipo wazi kabisa tunashindwa nini kuelewa. Sote tunajua hao wazungu plus wachina hakuna anayetupenda hata mmoja wote wana target zao tu huku afrika. But kwa hili la WHO mie naona mzee yupo sawa, Hiyo Organisation imekuwa nzembe sana kwa taarifa zao cha nusu nusu yaani ni kama hawajielewi kabsa nini wanafanya. Trump kupuuza taarifa za awali za ugojwa huu ni jambo la kawaida tu kwa mwanasiasa yoyote mfano Tz ya sasa. Lakini kama WHO wangetangaza mapema alert ya hili janga na kutoa miongozo wenda sote tungeepuka. Awali walisema hawawezi kulifanya kama janga la dunia sababu lipo China tu so walichokuwa wanasubiri ni kuenea dunia nzima ndo watangaze kama kilichotokea sasa ili waendelee kupiga pesa.
Sisi watu weusi China ametuhadaa sana yaan tumekuwa na ego furani hivi za kipumbavu sana na bora tungekuwa tunajaliana basi tupo na ego plus kuwekeana utemi then tunasema Mtendaji mkuu wa WHO kaonewa sababu ni mwafrika mbona awali hatukuliona hili au mbona hakuondoa pesa sababu kapewa uongozi mwafrika.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elezea basi wewe kile unachojua kuhusu hilo, hoja hupingwa kwa hoja.
 
Acha zako kuna mgawanyo wa majukumu. Ndio maana us anatoa mchango mkubwa WHO. Hivi WHO wanasema travel ban sio muhimu Trump ana initiate wewe ungemwitaje Trump?. Acha unafiki. Niga amefeli arudi kwao akale mirungi. Yaani miafrika sijui tukoje mbele ya ngozi nyeupe. Yaani chochote china walichokuwa wakimwambia ndio anasema kama mdori bila kufanya tafiti. Shenzy zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
....
The WHO ;
  • Claimed there is no human to human transmission
  • Said travel bans are not necessary
  • Praised China after they lied Covid-19 is under control
  • Told us to wash our hands and wearing mask is not necessary
....
... WHO ndio walisema hivyo mwanzoni!!!? Totally incompetent! Kibaya zaidi huyo Tedros (WHO DG) kageuka mpiga zumari wa wachina mabaguzi ya kutupa! Trump is right.
 
Naiunga mkono marekani WHO walificha taarifa kutahadharisha mapema aondoke tu.Tena haraka ni incompetent kama Dk Mwele Malechela wetu ambaye alileta uzushi Wa ugonjwa usiokuwepo Magufuli akamtimua halafu hao WHO wakamchukua sijui huyo Dk Mwele Makechela in hawara yake huyo incompent mkuu Wa WHO?

Aondoke upesi stupid.Namuunga mkono Trump
 
sasa wewe na Dr nani ana impact duniani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani chochote china walichokuwa wakimwambia ndio anasema kama mdori bila kufanya tafiti. Shenzy zake.
You have no proof whatsoever kwamba China ilikuwa ikimwambia Dr. Tedros kufanya kitu ana yeye anaact. By the way kila Nchi inapaswa kufanya tafiti zake na kujilinda accordingly. Kuna evidence kwamba CDC ya USA waliiona hii kitu mapema na wakaanza kuchukua hatua kimyakimya. Obama alionya kitu kama hii mapema kabisa lakini people did not listen at all au walipuuza. Nchi Kama South Korea na Singapore waliact faster.

Bottom line: hatuwezi kuwabebesha lawama WHO if somebody somewhere failed miserably to act timely, decisively and in a professional manner.
 
Atoke ni mjinga sana huyu jamaa..!

Kuficha taarifa za hatari ya huu ugonjwa kwa kuangalia maslahi ya china kunapelekea dunia kuingia kuzimu na hawa virusi.

Kwanini walichelewa kutoa tahadhari ya mapema kwa dunia kukaa mbali na China [emoji630] ili kutoa mwanya wa kushughulikia hawa virusi wakiwa China.

Kuna uzembe mkubwa umeigharimu dunia na maisha ya watu yanateketea kwasababu ya ujinga wa Mchina. Wachina ni watu wabinafsi kabisa kwenye hii dunia. Na inafaa dunia kuwawajibisha kwa uzembe walio ufanya wapuuzi hawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usipuuze hii taarifa ipo pia CNN

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hivyo ni vyanzo vya kijasusi vya wamarakani ndio walotoa taarifa hizo.

Kama ulikuwa hufahamu ni kwamba maabara yoyote inayofanya tafiti zake khasa zinazovuka mipaka, huwa zinafuatiliwa kwa udani ikiwemo watafiti wake.

Ndo maana hata zile maabara zinazofanya tafiti zinazohusu wanyama, zingine huweza kuwa "vandalised" na wanaharakani wa mazingira na watetezi wa haki za wanyama kwani nao hufanya kazi za kijasusi kugundiua kuna nini chafanywa ndani ya maabara hizo.

Majasusi walikuwa wakiwafuatilia wachina na maabara zao ile ya Wuhan na ile ya Marekani ambayo inafadhiliwa na wamarekani.

Sasa kila maabara ina protokali zake na wamrekani walianza kuona protokali zinakiukwa ikiwemo kuwashirikina interns ambao wengine ni kama huyo msichana.

Kumbuka ile maabara na fedha ambazo zilikuwa zikitolewa na wamarekani kufadhili utafiti lakini wachina wakawa pia wanatafiti popo wa Wuhan na maabara ya Wuhan.

Hivyo hawa wafatiti wa kichina walianza kufuatiliwa mienendo yao kwa kipindi kirefu.

Wamrekani wanafahamu kila kitu kuhusu kinachoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…