Ni vigumu kwa Mwafrika Dr Tedros Ghebreyesus kuendelea kuongoza WHO, Marekani yaondoa fedha za mchango nyuma ya pazia, yashinikiza Tedros aondolewe


Ndiyo, hiyo ilikuwa ni mwishoni mwa January ambapo WHO lizionya nchi zote wanachama juu ya seriousness ya COVID-19 na ikashauri hatua zote za kujikinga, kufanya testing na kufuata guidelines za WHO katika kukabiliana na COVID-19

Nchi za Korea Kusini na Singapore ambazo zimekuwa mfano wa nchi ambazo zilifuata maelekezo ya WHO tumeona jinsi idadi ya maam ukizi yalivyopungua katika nchi hizo.

Leo hii Korea Kusini tokea mwezi February idadi ya watu wanoambukizwa imeshuka kutoka watu 900 kwa siku hadi watu 30 kwa siku., hiyo yote ikiwa katika kufuata utaratibu wa "tressing and testing".

Hivi ni vielelezo tosha kwamba nchi wanachama zilikuwa zikifuata maagizo ya WHO kila mmoja kwa uzito wake.

Raisi Trump alianza ku-downplay hii kitu tangia mwezi January na alipoona mwezi march mambo yamekuwa mazito na idadi ya wagonjwa inaongezeka akaanza kuchukua hatua ingawa jamaa wa CDC nao walikuwa wakishauri mapema juu ya hatua za kuchukuliwa kukabillana na COVID-19

Tuangalie hii suala kwa mizani ya kihalali na sio zile za kutumia mawe ya zege.
 
Mjumbe WHO ni kazi yao kutoa tahadhari ndio maana wanalipwa sasa kusema Obama sijui nani unakosoa Obama ni nani WHO mpaka atoe tahadhari?. Hebu toka hapo utangaze wagonjwa mtaani mwako hata iwe kweli uone. Wapo watu walioteuliwa maalumu kuhakikisha wanatoa taarifa hawa wasipowajibika sote tunakufa.
 
Wachina hawafai kabisa I think waneficha mengi kuhusu huu ugonjwa na takwimu madhara yake dunia inahangaika na Sasa wanawatesa wa Africa. China awajibishwe tu kwa hili Tena mwanzo ingetakiwa wajiweke quarantine.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

China were spot on and Trump acknowledged it😎. Hizi mbwembwe mpya ni kiwewe maana hana clue ya nini afanye na wenge la kuchapwa kwenye uchaguzi limeshaanza kuset in

 
Sawa lakini hii tabia ya Waafrca kuacha mambo ya msingi na kuegemea kwenye siasa za Uchina kwa ujira wa vimisaada uchwara eti havina masharti ndio madhara yake.Binafsi naona huyu mkuu alichemka sana kujua ukweli na akabaki na Wachina,sasa lazima hili limgharimu.
Bahati mbaya huyu jamaa aliwahi kuwa waziri wa mabo ya nje wa Ethiopia ko anajulikana ni mwanasiasa pure na kwa nature ya waafrica is likely aliegemea Uchina
 
Tena WHO iliwasaidia kisa tuu Wachina ni wawekezaji na watoa misaada uchwara kwa viongozi wasitaka kufikiri wa huku Africa,sasa bwana Tedros akawa analipa fadhila.Trump kaza hapo hapo kwa nini atuteketeze na sisi tusio husika?
 
Sina cha kuongeza. Well said. Kudos 👏
 
Sio tu kuwa inamwambia lakini huyu dr ni mwanasiasa na amewhimkuwa foreign minister wa huko kwao,kwani nani hajui kwamba wachina ndio wawekezaji wakubwa Ethiopia na africa kiujumla na viongozi wa Afrika wanawategemea wachina kwa vimisaada uchwara? Huyu amechemka kwa kulipa fadhila Uchina na kuhatarisha maisha yetu,haijalishi rangi kama anajua Waafrika hatutakiwi kwa nini afanye makosa ya wazi na uzembe kiasi hiki?
 
Kila siku alikuwa kwenye Tv anajivuta vuta,mara ooh tusifunge mipaka,mara ooh china itaudhibiti yaani wanakuja kutoa alert duniani ugonjwa umefikia mataifa,hii haikubaliki ajiuzulu au wamuondoe tuu
 
WHO ipo tu kimuundo na jina, hivyo kuilaumu kwamba haiko makini ktk kutoa taarifa zake juu ya huu ugonjwa ni kuwaonea tu.
Nchini nyingi na hasa China hazina uwazi juu ya ugonjwa covid 19 hivyo ilikua ni kazi ngumu kupata taarifa zq jinsi gani ugonjwa huo unavyo ambukizwa na kuenea mpaka pale ulipo ingia Ulaya ndio hapo uwazi juu ya ugonjwa huo ukawepo.
 
Nchini Uingereza mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi wa nje la MI16 bwana John Sawer amesema kwamba China ilificha kwa dunia taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa COVID -19.

Jasusi Sawer amesema ujasusi ni kupata taarifa ambazo zimefichwa usizipate kutoka kwenye nchi na wahusika wengine. Lakini kulikuwa na ufichwaji wa taarifa za awali zilizokuwa zikitolewa tangu mlipuko uanze mwezi Disemba na januari kwa nchi za magharibi na Marekani.

Madai hayo ya jasusi huyo mbobezi yanalingana na madai ya majasusi wa Marekani na vyanzo vingine mbalimbali ambao walimpatia raisi Trump taarifa kwamba pamoja na kirusi COVID -19 kutokea kiasili lakini kuna kila dalili kwamba kirusi huyo alitengenezwa kwenye maabara ya Virolijia mjini Wuhan. Niliposoma kipande hiki nikajiridhisha kama hapa kuna mchezo wasiasa ambao US Anaufanya Dhidi Ya UCHINA Kwahio Jasusi Tena Mbobevu Wa UK Apingane Na Mwanawe Wakumzaa Kabisa Ambae Ni US katika Suala La Maslahi ?!


US kama Kaamua Kujitoa Ajitoe Asitafte Huruma Na Tention Zawatu Hapa

Wanajua Kama wamekurupuka Eeeh[emoji23][emoji23]

Sent using My COVID-19
 
Ungekua unaelewa maana ya utafiti wala usinge andika hichi ulicho kiandika
Sent using My COVID-19
 
Kama mfadhili mkuu wa WHO (Marekani) anataka huyo mkurugenzi aondoke basi lazima ataondoka tu.

Hata hao viongozi wa Africa wanaomtetea Dr Tedros yaani kina Kagame, Buhari na Ramaphosa wanafahamu vizuri hilo.
Nnachoshangazwa hapa kama US Kaamua Kusepa SiAsepe tu Maswala Yakutaka Sijui Nani Aondolewe Yanaanzia Wapi Sasa ?!

US Anataka Amueke Mtu Wa Ndio Mzee[emoji16][emoji23][emoji3]

Sent using My COVID-19
 
Trump anjijua mwenyewe Wakati ana ambiwa alikua hakubali sasa anahangaika tu pumbav zake aache siasa kama kaamua kusepa nakukata msaada akate tu hakuna namna ss.

Sent using My COVID-19
 
Kama ulitaka janga moja ambalo linatafuna sehemu moja liekwe kama janga laduni Mbna Hukusemea Kuhusu EBOLA ?! Au Sababu Ebola Inawaua Waafrika Tu Natena Wakongo Kama mwanasiasa lazma adharau hatua zamwanzo sasa Tram ndio anakula dharau zake sasa

Aache kulia lia

Sent using My COVID-19
 
Mhh, wale red brigade wa ufipa wanasemaje kuhusiana na huu ujasusi wa kimataifa??
 
We hujui propaganda za wazungu wanataka kuibebesha Uchina mzigo, kama wao walikuwa na taarifa hizo mapema kwanini hawakuchukua tahadhari za kukinga nchi zao? Trump anajua corona inamshushia hadhi maana alijigamba sana, sasa wanatengeza propaganda za kuilaumu China ili alinde kiti chake
 
We hujui propaganda za wazungu wanataka kuibebesha Uchina mzigo, kama wao walikuwa na taarifa hizo mapema kwanini hawakuchukua tahadhari za kukinga nchi zao? Nashangaa sana asee

Turampet aache kulialia bwege yule.

Sent using My COVID-19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…