Ni vipi naweza kupata Hati ya Tabia Njema?

Ni vipi naweza kupata Hati ya Tabia Njema?

Mkuu ni kweli.

Infact, siyo rekodi ya Tabia njema japo wengine wanaiita hivyo. Bali ni criminal record (rekodi ya uhalifu) .

Taasisi zingine zinahitaji kujua kama hujawahi kukutwa na kosa lolote. Achana na kushutumiwa, bali ile umehukukiwa kabisa.

Rekodi ile huitumia kujua mienendo yako. Kisha wanakuajiri.

It is a serious thing.
Asante sana mkuu kwa maelekezo yako mazuri sikuwa najua kabisa hiki kitu.
 
Habari za usiku ndugu zangu.

Kilicho nileta hapa ni kujua jinsi gani naweza pata hati ya tabia njema. Mahali inapopatikana, vitu ambavyo natakiwa niwe navyo na gharama.
Nahitaji sana hii kitu kuweka mambo sawa kazini. Napitia Comments za wadau nijue pa kuanzia.
 
Hati ya tabia njema Inapatikana Wizara ya mambo ya ndani Kwa hapa tz makao makuu yako posta

Unachotakiwa kufanya ni kufika pale ukiwa na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa then kuna form ya kujaza ..afu utalipia km 2000 tuu lakini wanakupa control number unaenda kulipia afu wataku scan kidole gumba kujiridhisha km hujawahi kufanya uhalifu wowote ...then baada ya siku km.moja hv utaitwa kwenda kuchukua Hati yako
 
Ni Polisi Makao Makuu Dar nje pale kwenye Tents,watakuchukua Alama za Vidole(Finger Prints) kisha baada ya siku mbili au tatu utaenda kuchukua Hati yako(Police Clearance Report),uende na Passport Size,kwa mikoani unaweza kuipata Central Police Stations
 
Nenda wizara ya mambo ya ndani?
Nenda na kitambulisho chako
Nenda na document inayoonesha wewe kuhitaji hiyo certificate of clearance ..basi
Gharama yake kulipia Bank ni 2000 sijui kama sahv imeongezeka

Ova
Document hiyo iwe ni kitambulisho Cha Taifa au pasipoti pamoja na picha mbili na elfu 2500 kwenye simu yako ukienda watakupa control number utalipia halafu watakuchukua fingerprint kisha siku hiyo hiyo unapewa certificate yako

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom