Ni vitu gani muhimu ambavyo watu wengi hawataki kuvitumia na hata wakiwa navyo huvipuuza?

Ni vitu gani muhimu ambavyo watu wengi hawataki kuvitumia na hata wakiwa navyo huvipuuza?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,406
Reaction score
19,375
Kwangu mimi

1. Mikanda ya kwenye gari - ajali zikitokea huwa inasaidia sana, Cha ajabu nguvu kunwa inatumika kukumbusha watu kutumia mikanda lakini wao hawana muda na mikanda

2. Condom - watu wameumiza vichwa sana walianza na utumbo wa mnyama mpaka kufikia hizi condom, lakini ajabu watu huzipuuza na wengi kuishia kupata magonjwa yanayowatesa sana na mimba zisizotarajiwa

3. Hodi - Kuna watu wameturusha vichura chura bila kupenda kwenye vyoo, Yani mtu anajua kabisa mlango wa choo ni mbovu lakini yeye akifika anasukuma tu

Endeleeni
 
Nikiwa mabibo hostel miaka fulani, ilikuwa kuna watu wakitoka kula nje vile vi chenchi mia mia wakawa wanatumia kupima uzito pale nje ya gate.

Binafsi nlikuwa nawapinga sana, nlikuwa naona kutoa vile vi mia mia ni kupoteza hela za bure
 
Kutumia asali,kunywa maj unavyotakiwa,kula mboga za majan inavyotakiwa
 
watu wengi wanapenda kupuuza tahadhali zinazogonga kengere kichwani.

mfano unatoka kwako,kengere inalia kichwani,ongeza mafuta kwenye gari,unajikausha kibishi ngoja nifike mbele kidogo pale airport ntaongeza.unafika katikati gari inazima,unaanza kujilaumu.mbaya zaidi unatakiwa uisukume itoke barabarani[emoji26][emoji26][emoji26].

siku hizi nimeanzisha zoezi la kuisikiliza sauti hiyo,nimegundua ukiiheshimu haikuachi mkono itakukumbusha kila jambo ambalo linahitaji tahadhali.mpaka wenzangu huwa wananiambia nna mdomo mchafu.
 
Vyombo vipya vizuri vizuri vya kupikia kwenye kabati. Vinaguswa vya zamani tu!
 
Back
Top Bottom