Nimewahi miliki vw touran mwaka 2014 mpaka 2016 ni gari nzuri, ipo comfortable, speed juu body ni nzito quality ya hali ya juu sana sio kama chuma uchwara Toyota. Lakini siwezi kumshauri mtu anunue hiyo gari. Ilinifanya niyaogope magari ya mjerumani kwani ni ugonjwa wa moyo.
Wife aligonga kidogo taa ya mbele 1 ikapasuka sikuweza pata Dar wala Nairobi, nikapata south Africa mjini Johannesburg. Nilinunua pair kama laki 4 ya bongo,shock ups pia nilipata huko.
Ilipata tatizo la gearbox ku-change gears tatizo ambalo ni very common kwa vw za 2003 mpaka 2006 zinazotumia DSG transimition. Ilitakiwa nipate gearbox nyingine au niweke gari juu ya mawe. Pia ilikua na tatizo la check engine light kuwaka mara kwa mara, airbag erro light kuwaka nk .Uwezo wa kuagiza spare nilikua nao lakini ni shida, kama unanua vw basi at least iwe moja ya zile ambazo zipo common Tanzania kama toureg.