bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,565
- 2,966
Habari wanajamii,
Kutokana na malezi au asili ya mtu kunapelekea kuwepo kwa aina mbalimbali za binadamu wenye tabia za kufanana.
Katika uzi huu nitajikita kueleza kinaga
ubaga cha type ya binadamu ambayo kitaalamu wanaitwa sycophant.
Kama una udadisi utakuwa ushawahi kutana na psychopath hadi uzi upo humu jamii forum, naeleza hivyo ili usije changanya baina ya watu wa aina mbili hizi hawa psychopath wengi utawakuta magerazani kutokana na tabia zao ukatili na kutokuogopa hivyo mara nyingi kujikuta wapo chini ya ulinzi baada kuzuru watu wengine, shida ni kwamba kuna baathi ya watu wakubwa ambao wana ka percent ka u psychopath ambao wanajificha kuenyesha makucha yao.
Hawa wanaojificha ni hatari Zaidi kwani katika nyadhifa ambazo wamezishika wanafanya maamuzi yao bila kujali ubinadamu au huruma kwa binadamu mwenzao, in short haweelewi suala lolote kuhusu huruma na kuthamini utu wa binadamu mwenzao hivyo maamuzi yao yanaumiza watu wengi sana.
Sasa turudi kwa Sycophant huyu ni binadamu ambaye yeye kama yeye hawezi akasimama kama yeye na mawazo yake bali hutafuta mtu wa kumuigiliza na kumuunga mkono asilimia mia, yaani huyu hawezi pinga hata kidogo maamuzi ya mtu ambaye anataka mkopi, hawa ndio Mr yes, na wapo kila kona hapa ngoja nieleze baadhi ya mifano yake
Nenda acirema utawakuta wakiongozwa na lile zee kila siku kulia kama ndege, nenda nopilifi utawakuta wanadiriki kushangilia mkuu wao anavyotandika watu risasi.
Mara nyingi sana haya Sycophant wakipewa majukumu na boss wao huwa wanafanya kwa kupitiliza ili mradi wametimiza bila kujali hasara kwa wenzao au kwa jamii.
Pinga kuwa sycophant na watambue mapema ili kukabiliana nao.

- Kama una rafiki yako ambaye hadi anakuiga staili ya kuvaa tokea ujuane nae, basi tambua huyo ni Sycophant ajae, wengine huenda mbali hadi kuiga uongeaji, swaggz, kutembea.
- Kama una rafiki, huko makazini mfanyakazi mwenzenu ambaye yeye kila asemalo boss lazima akubali, hawezi pinga jambo ambalo boss kasema yeye siku zote yupo upande wa boss, anapenda kumsifu boss sana mara nyingi boss akiwa yupo ndo anamwaga sifa kwa boss mpaka basi,
- Hupenda kuengea kwa niaba ya mtu ambaye wanamfwata, hii utakuta katika maongezi wanavaa uhusika wa mtu mwingine na kutoa maamuzi kama ni ya huyo mtu, au kukataa point kwa sababu wanazani wamwigaye atakataa pia.