MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Leo nilitembelea page ya Foods for children nikaona video ikionyesha mji wa Karatu na kushangazwa na jinsi ulivyopangiliwa. Ninadhani huu ni mji ambao hata ukisema upanue barabara hutakuwa na haja ya kuanza kubomoa nyumba za watu kama ilivyo Dar Es Salaam na miji mingine mikubwa.
Lakini pia inawezekana hii hali imechangiwa na wananchi wa hapo kufuata sheria na sio kujenga hovyo kama watu wa Msimbazi walivyojenga bondeni. Wananchi kujenga bila kufuata utaratibu pia ni changamoto kubwa sana. Tujifunze kwa watu wa Kartu.
Kasoro ya watu wa Karatu ni kupenda sana upinzani. Tangu mwaka 1995 wao wamekuwa wakiichagua CHADEMA hadi mwaka 2020 walipoamua kumchagua mgombea wa CCM na kisha mwaka 2025 kumrudisha tena bungeni.
View: https://web.facebook.com/share/v/1B9G2gdYiV/