Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Hili la kuomba kodi ikatwe kwenye mita moja tu linatakiwa lifanyike TANESCO au TRA?Nyumba yangu Ina mita za Luku nne tangu uanze utaratibu wa kulipia kodi Kila mwezi nimenda na kuandika barua mara kumi ikatwe moja na mpaka leo hawajaja kuhakiki.
Mi rushwa sitatoa na siku ya siku fedha za ziada zitarudi
TANESCO UBUNGO
Hahaha,,,, [emoji13]
Utajikuta umeuza Ng'ombe ili kupata pesa ya kudai Kuku.
Hili la kuomba kodi ikatwe kwenye mita moja tu linatakiwa lifanyike TANESCO au TRA?
Hii hii, kama wamekuunguzia kitu kadai haki yako MkuuTanesco hii hii
Danganya toto sio, ili watu wawe na imani"Dear mteja hicho kipengele tulikiweka tu geresha kifupi mtafidiwa kiama"Wenu katika kuangaza taanesko
Yawezekana kuwa watu hawajui pamoja na wewe mleta thread kuwa wapo wateja wa TANESCO waliolipwa fidia kutokana na tatizo la umeme lililosababisha na uharibifu wa mali katika hali ambayo mtumiaji hakuhusika.Wakuu kwema?
Kulingana na Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, mteja ukipata hasara kutokana tatizo la umeme, TANESCO inatakiwa kumfidia mteja huyo. Kipengele hiki kinasema;
"Kuwafidia wateja pale ambapo tatizo la umeme limesababisha uharibifu wa mali baada ya kuwa imehakikishwa kwamba tatizo hilo halikusababishwa kwa hali yoyote na mtumiaji wa umeme."
Mara ngapi umewahi kupata hasara kutokana na tatizo la umeme? Umewahi kudai fidia kutoka na hilo? Au ndio tunamuachia Mungu?
CC TANESCO