SoC01 Ni wajibu wetu kujitoa kuwasaidia watu wenye mahitaji muhimu katika jamii

Stories of Change - 2021 Competition

Kifurukutu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
4,641
Reaction score
6,694
JF

Katika jamii kuna makundi ya watu mbalimbali, wapo watu wanaojiweza kumudu mahitaji yao yote lakini pia kuna makundi ya watu hawajiwezi kumudu mahitaji yao ya kila siku katika maisha

Mahitaji muhimu katika maisha ya mwanadamu ni Chakula, malazi na mavazi,, katika jamii yetu hii kuna watu wanakosa mahitaji hayo

Makundi ya watu wenye uhitaji zaidi ni
•watoto yatima
•waanga wa majanga mbalimbali
•Makundi ya watu wenye ulemavu
•Wazee
•Wakimbizi
kwa uchache makundi hayo hapo juu yanakosa mahitaji muhimu ya kibinadamu

Hebu jaribu kujiuliza wewe hapo unayejiweza, utayamudu vipi maisha endapo huna chakula?

maisha yataenda vipi bila kuwa na sehemu ya kuishi na nguo ubadilishe kila siku?

Kama ulikuwa hufahamu sasa naomba ufahamu kwamba mimi na wewe hapo tunaowajibu (lazima) kuwasaidia watu hawa wenye mahitaji muhimu katika jamii

Ni muhimu sana kuwasaidia watu hawa kwa sababu zifuatazo
•Kulinda na kuheshimu utu..hakika utu huifadhiwa na upatikanaji wa chakula malazi na mavazi!
• upendo, amani na mshikamano vinadumishwa katika jamii
• Haki za watu wengine kuishi zinaheshimika kupitia msaada wako wewe
• Kiroho,, Mungu naye hutukumbuka na kutuongezea zaidi pale tulipopunguza
• Misaada yetu inapunguza makundi tegemezi katika jamii
• Hupunguza umasikini katika jamii

Ni mtu wa aina gani anatakiwa kuwasaidia watu wenye mahitaji?
Mtu yoyote yule mwenye uwezo anaweza kumsaidia mtu mwenye uhitaji kwani waswahili husema wema usizidi uwezo hivyo saidia kadili ya uwezo wako,,, uwe na kidogo au kikubwa wewe saidia tu

Hapa Tanzania watu wenye mahitaji wengi humkumbuka sana marehemu Reginald Mengi..Hakika huyu mtu aliwajali watu wenye uhitaji

Ni zamu yetu sasa, mimi na wewe tujitoe kuisaidia jamii kwa kuwagusa hawa watu wenye mahitaji

Tutoke tuwatembelee yatima na wazee katika vituo vya kulea wazee na watoto yatima vilivyo karibu nasi

Tutoke sasa tuzitembelee public schools huko kuna watoto wengi wenye mahitaji wanatusubiri tuwawezeshe wafanikishe ndoto zao kielimu na kimaisha

Mwisho, ni wajibu wa kila mtu anayejiweza kuwasaidia watu wenye uhitaji,, pia serikali na taasisi binafsi hazina budi kushirikiana kuhakikisha zinayasaidia makundi haya muhumu katika jamii

nawasilisha
 
Upvote 14
Kwani kuna mtu amekulazimisha mkuu? Ila tambua kua,Dunia ina zunguka,maisha ni kama gwaride,wambele anaweza kua nyuma na wanyuma anaweza kua mbele,

Ndio maana wahenga wanasema hakuna ajuaye kesho ya mwenzake na wema hauozi.
endelea kujitolea kwani unatulazimisha sasa
kila mtu anamisingi yake katika maisha
 
Msaidie mtoto asante sana muanzisha mada mtoto anaitwaBakari Omary ambaye amezaliwa mgongo wazi,anahitaji mkubwa wa wheelchair na pampas.ana umri wa miaka 13,anasoma darasa la sita wheelchair aliyokuwa anaitumia imechoka na kuharibika.sasa hivi anajivuta chini hawezi Tena kwenda shule anahitaji msaada wa haraka.Mwenye moyo wa kumsaidia anaweza muwasiliane na mratibu Grace kwa namba 0754407588. Mumewe amemkimbia baada ya kuzaa mtoto huyo anahangaika mwenyewe na watoto wanne kwa kujishughulisha na biashara ndogondogo.
IMG_20210714_125155_596.jpg
 
Msaidie mtoto asante sana muanzisha mada mtoto anaitwaBakari Omary ambaye amezaliwa mgongo wazi,anahitaji mkubwa wa wheelchair na pampas.ana umri wa miaka 13,anasoma darasa la sita wheelchair aliyokuwa anaitumia imechoka na kuharibika.sasa hivi anajivuta chini hawezi Tena kwenda shule anahitaji msaada wa haraka.Mwenye moyo wa kumsaidia anaweza muwasiliane na mratibu Grace kwa namba 0754407588. Mumewe amemkimbia baada ya kuzaa mtoto huyo anahangaika mwenyewe na watoto wanne kwa kujishughulisha na biashara ndogondogo.View attachment 1854343
Pole sana kwake nitamsaidia kulingana na uwezo wangu

Lakini pia endapo nikishinda mpambano huu, hiyo wheelchair nitainunua nimkabidhi,, piga kura sasa niibuke kidedea
 
JF

Katika jamii kuna makundi ya watu mbalimbali, wapo watu wanaojiweza kumudu mahitaji yao yote lakini pia kuna makundi ya watu hawajiwezi kumudu mahitaji yao ya kila siku katika maisha

Mahitaji muhimu katika maisha ya mwanadamu ni Chakula, malazi na mavazi,, katika jamii yetu hii kuna watu wanakosa mahitaji hayo

Makundi ya watu wenye uhitaji zaidi ni
•watoto yatima
•waanga wa majanga mbalimbali
•Makundi ya watu wenye ulemavu
•Wazee
•Wakimbizi
kwa uchache makundi hayo hapo juu yanakosa mahitaji muhimu ya kibinadamu

Hebu jaribu kujiuliza wewe hapo unayejiweza, utayamudu vipi maisha endapo huna chakula?

maisha yataenda vipi bila kuwa na sehemu ya kuishi na nguo ubadilishe kila siku?

Kama ulikuwa hufahamu sasa naomba ufahamu kwamba mimi na wewe hapo tunaowajibu (lazima) kuwasaidia watu hawa wenye mahitaji muhimu katika jamii

Ni muhimu sana kuwasaidia watu hawa kwa sababu zifuatazo
•Kulinda na kuheshimu utu..hakika utu huifadhiwa na upatikanaji wa chakula malazi na mavazi!
• upendo, amani na mshikamano vinadumishwa katika jamii
• Haki za watu wengine kuishi zinaheshimika kupitia msaada wako wewe
• Kiroho,, Mungu naye hutukumbuka na kutuongezea zaidi pale tulipopunguza
• Misaada yetu inapunguza makundi tegemezi katika jamii
• Hupunguza umasikini katika jamii

Ni mtu wa aina gani anatakiwa kuwasaidia watu wenye mahitaji?
Mtu yoyote yule mwenye uwezo anaweza kumsaidia mtu mwenye uhitaji kwani waswahili husema wema usizidi uwezo hivyo saidia kadili ya uwezo wako,,, uwe na kidogo au kikubwa wewe saidia tu

Hapa Tanzania watu wenye mahitaji wengi humkumbuka sana marehemu Reginald Mengi..Hakika huyu mtu aliwajali watu wenye uhitaji

Ni zamu yetu sasa, mimi na wewe tujitoe kuisaidia jamii kwa kuwagusa hawa watu wenye mahitaji

Tutoke tuwatembelee yatima na wazee katika vituo vya kulea wazee na watoto yatima vilivyo karibu nasi

Tutoke sasa tuzitembelee public schools huko kuna watoto wengi wenye mahitaji wanatusubiri tuwawezeshe wafanikishe ndoto zao kielimu na kimaisha

Mwisho, ni wajibu wa kila mtu anayejiweza kuwasaidia watu wenye uhitaji,, pia serikali na taasisi binafsi hazina budi kushirikiana kuhakikisha zinayasaidia makundi haya muhumu katika jamii

nawasilisha
Mkuu ubarikiwe kwa bandiko maridhawa
 
Back
Top Bottom