Pre GE2025 Ni wakati muafaka na sahihi kwa David Kafulila kurejea Bungeni mwaka 2025

Pre GE2025 Ni wakati muafaka na sahihi kwa David Kafulila kurejea Bungeni mwaka 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Kila jambo na majira yake na wakati kwa kusudi maalumu chini ya mbingu. Nafikiri sote tunamfahamu vyema Mheshimiwa David Kafulila,tunafahamu uzalendo wake kwa Taifa letu,uchapa kazi wake, upendo wake kwa Wananchi. Tunafahamu vyema na kwa undani uwezo wake wa kujenga hoja na kuitetea hoja,tunafahamu bila shaka uelewa wake wa masuala mbalimbali hususani ya kiuchumi, biashara,fedha n.k.

Sote ni wazi tunakubaliana kwa pamoja kuwa Chuma David Kafulila ni mtu aliye muadilifu,muaminifu na mtu aliyenyooka kama rula kitabia.hanaga kupinda pinda. Ni mtetezi wa kweli wa Taifa letu kama ilivyo kwa mama yetu na Jemedari wetu Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Sote tunatambua ni mtu mnyenyekevu,mstarabu na mtulivu sana kiongozi.

Sote tunatambua kuwa ni mtu anayeacha alama za kiuongozi kila eneo anapopewa nafasi na kuaminiwa kutumikia Taifa lake.tumeona tangia akiwa mbunge,RAS Songwe,RC Simiyu na sasa mkurugenzi Mkuu wa PPP.

Hivyo naona ni wakati muafaka na sahihi na wakati wake wa kuweza kurejea Bungeni hapo mwakani panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu.ni wakati wa kulitumikia Taifa lake na kumsaidia Mheshimiwa Rais katika masuala mbalimbali ya kisera. Ni dhahiri sauti ya Chuma David Kafulila inahitajika Bungeni.ni muhimu watu aina yake wakawa sehemu ya bunge.

na kama ikimpendeza Jemedari wetu Mama Samia Basi anaweza kumvuta ndani ya Baraza lake la Mawaziri atakaloliunda mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi na yeye kuwa amepita na kushinda Urais kwa kishindoo.maana watanzania wanakiu kubwa sana ya kumpa kura za ndio kwa fujo kama shukurani kwa kazi kubwa aliyowafanyia.

Natambua pia watu aina ya David Kafulila huwa wakati mwingine wanapigwa vita sana,kuchukiwa bila sababu ,kusingiziwa uongo,kupakwa matope,kusulubiwa na mikuki ya maneno ya kizushi na uongo na watu wenye uchafu na Makando kando au wasiopenda kusikia ukweli masikioni mwao. Lakini tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutupatia Rais Samia Jemedari wetu imara na shupavu ambaye yeye amejaa upendo mkubwa sana kwa watu wazalendo na wachapa kazi aina ya David Kafulila na ndio maana ameendelea kuwa naye na kumuamini mpaka kumpatia Ukurugenzi wa PPP. japo kuna watu hasa wabaya wa Kafulila wanatamani au wasingependa kuona akipata nafasi yoyote ile katika serikali ya Rais SAMIA maana inakuwa inawapa hofu na uoga mkubwa sana.

Watanzania tunapaswa kujenga utamaduni wa kuwatia moyo, kuwaunga mkono,kuwatetea ,kuwasemea wazalendo aina ya Daktari Mama Samia Suluhu na David Kafulila na wengine wengi.kwa kuwa wazalendo siku zote hupigwa vita ,kushambuliwa,kuumizwa,kutengenezewa ajali,kuchafuliwa na kuchukiwa sana bila sababu ya aina yoyote ile. Tumlinde na kumtetea Rais wetu na wale wote wanaoonyesha dhamira na muelekeo wa uzalendo kwa Taifa letu kwa dhati ya mioyo yao. David Kafulila Ni mzalendo na mchapakazi na anastahili kuungwa mkono.

Ngoja niweke kalamu yangu chini ili kutorefusha andiko na kuwachosha wasomaji.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Umetoka kwa mama sasa hivi upo kwa Kafulila!
Yajayo yanafurahisha..!🤸
Mimi nipo na wazalendo wote ambao naona wanaweza kumsaidia mama yetu na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan. Unajuwa ngoja nikwambie kitu ephen wangu ,ni kuwa Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ni mzalendo kwelikweli na mchapa kazi sana na sote tunaona kazi kubwa na nzuri anayoifanya.

Hivyo basi ili mama yetu afanikiwe zaidi inatakiwa azungukwe na kuwa na watu sahihi na wazalendo katika kila eneo la kuwatumikia na kuwahudumia wananchi.watu watakao kuwa wanazungumza lugha anayozungumza Rais wetu,watakao kuwa na maono aliyonayo Rais wetu kuipeleka mbele Nchi yetu.watu na wazalendo hao ndio mfano David Kafulila.

ephen wangu embu fikiria mfano Rais anatafuta pesa kwa jasho kubwa halafu apeleke sehemu kwa ajili ya wananchi kujengewa kituo cha afya au kupatiwa maji safi na salama ya kunywa ,halafu pesa zile zinafika kule zikaliwa na fisadi moja na wananchi wakakosa huduma.huoni kuwa itakuwa ni kumchonganisha Rais na wananchi? Huoni itakuwa ni kukwamisha juhudi za serikali na dhamira njema ya Rais wetu.

Ok ngoja niishie hapa ephen maana najuwa hupendi maandiko marefu .nami sipendi kuukwaza moyo wako bali nataka kukupa furaha na raha muda wote.
 
Anabidi agombee urais 2025 maana anafaa Sana kumpokea mama

Watu wote tutabugujikwa machozi ya furaha ya mama kumuachia kiti 2025.
2025 tunakwenda na Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan. ambapo tunaamini atamjumuisha pia David Kafulila ndano ya Serikali yake.ambapo naamini wala hatajuta kwa uamuzi huo.
 
Mama anaeleweka sana ndio maana naendelea kumuunga mkono kwa nguvu zangu zote.
Mama yenu bado anataka uraisi pamoja na kushindwa kudeliver

kwekli bongo kichwa mwendawazimu

Juzi alikuwa kwa hamonizer baada ya kuwakimbia wafanyakazi siku ya mei mosi

Nakumbuka miaka Ile wakati wa mgomo mkubwa wa chuo kikuu mzee mwyinyi aligima kuonana na Wanachuo akaibukia kucheza isambe na Kanda bongomam

Wakati huo Lucas bado hujazaliwa
Kama ulizaliwa ulikuwa kwenu huko Rungwe unachunga mbuzi.
wakati watoto wa mjini tusio ccm tunakula bata
 
Mama yenu bado anataka uraisi pamoja na kushindwa kudeliver

Juzi alikuwa kwa hamonizer baada ya kuwakimbia wafanyakazi siku ya mei mosi

Nakumbuka miaka Ile wakati wa mgono mkubwa wa chuo kikuu mzee myinyi aligima kuonana na Wanachuo akaibukia kucheza isambe kwa Kanda bongomam

Wakati huo Lucas bado hujazaliwa
Kama ulizaliwa ulikuwa kwenu huko Rungwe unachunga mbuzi.
wakati watoto wa mjini tusio ccm tunakula bata
Kwanza uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais anayeendelea kuchanja mbuga na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania kutokana na uchapa kazi wake. Wakati wa mei Mosi alikuwa nje ya nchi kikazi. Hata hivyo watumishi wa umma wanatambua kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Rais kuboresha maisha yao,ikiwa ni pamoja na kuwapandisha madaraja kwa mserereko,kulipa malimbikizi yao ya madeni,kuwapandisha mishahara hasa wale wa kimo cha chini n.k.
 
Kwanza uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais anayeendelea kuchanja mbuga na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania kutokana na uchapa kazi wake. Wakati wa mei Mosi alikuwa nje ya nchi kikazi. Hata hivyo watumishi wa umma wanatambua kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Rais kuboresha maisha yao,ikiwa ni pamoja na kuwapandisha madaraja kwa mserereko,kulipa malimbikizi yao ya madeni,kuwapandisha mishahara hasa wale wa kimo cha chini n.k.
Propaganda na ukweli ni vitu viwili tofauti
Waulize watumishi wa umma wanaostaafu nyakati hizi Hali zao zikojje?
 
Back
Top Bottom