Ni wakati muafaka sasa Alikiba ajikite kwenye kuimba kaswida, aachane na bongo fleva.

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Najua huku kuna wapambe wa karibu na Alikiba, King Kiba.

Najua pia King Kiba ni muumini mzuri tu wa dini yake ya kiislam, bila shaka anafuata mafundisho yake ya kidini vizuri. Ni wakati muafaka sasa ajikite kwenye kuimba nyimbo za kuitukuza imani yake na mungu wake, hii bongo fleva imemkataa. Na sio imemkataa, imefika mwisho.

Jambo lolote linalohitaji nguvu kama kucheza mpira au ngumi na akili kama kutunga nyimbo na kuimba hua lina muda linaisha maana nguvu huisha na akili huchoka kutokana na mabadiliko ya mwili na umri.

Alikiba akili yake ya utunzi wa nyimbo umefika mwisho, sasa ajikite kwenye kutunga nyimbo za kidini hizi za bongo fleva zimekataa. Wakati ni ukuta.

Niliwahi kushauri pia kuhusu Diamond https://www.jamiiforums.com/threads...kuimba-kwenye-bar-grocery-za-mitaani.1562458/

Huu ni ushauri wangu wa bure.
 
Mkuu umeongea kweli kabisa Wala hujapepesa macho huyu jamaa wale ambae hatumkubali Mondi tumempausha sanaaaah tu! Ila moyoni tunajua anapuyanga tu... Kuanzia Rockstar na hiyo MARATHONI ni za viwango vya chini sana angalau hata CHIBONGE ya Mario na wenzie huko!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…