Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Ukweli ulio wazi ni kuwa Zitto kwa sasa hana mchango wowote kwenye siasa za upinzani za kutaka mageuzi hapa Tanzania, zaidi anachopambania ni maslahi yake binafsi kupitia serikali ya CCM chini ya utawala wa mama Samia. Jambo hilo sio afya kwa mustakabali wa malengo ya ACT hususani kwa upande wa Zanzibar.
Ni kweli Zitto ni muasisi wa ACT na ndio aliwakaribisha wafuasi wa CUF kuhamia ACT na kuifanya ACT kuwa na nguvu upande wa Zanzibar na hapo hapo CUF kufa kifo cha mende kisiasa. Kwa kifupi sana kifo cha CUF zanzibar kimeinufaisha ACT na kifo cha CUF Tanzania bara kimeinufaisha zaidi CHADEMA.
Kama zilivyo siasa za Zanzibar ambapo mipango huweza kubadili kila wakati lakini malengo hayajawahi kubadilika milele, kwa muelekeo huo wa Zitto kutaka kujikomba kwa utawala wa mama Samia, wafuasi wa ACT kwa upande wa Zanzibar wanaweza wasiwe na mwisho mzuri ikiwa wataendelea kupelekeshwa na siasa za Zitto zenye malengo binafsi ya kujipendekeza kwa watawala.
Kwa mfano leo hii Zitto hawezi tena kutamka chochote kuhusu kudai katiba mpya. Mtu wa namna hii ana msaada gani kwa siasa za mageuzi kwa upande wa Zanzibar?
Kupitia bandiko hili ninapenda kuwapa ushauri na angalizo muhimu wafuasi wa ACT kwa upande wa Zanzibar kuanza kuwa makini dhidi ya Zitto na siasa zake. Siasa zake kwa sasa zina mlengo wa kuunga mkono harakati zote za CCM kupitia serikali ya mama Samia, na nyingi katika hizo harakati zina mchango hasi katika siasa za mageuzi kwa aina ya upinzani Zanzibar.
Heri nusu shari kuliko shari kamili.