PreGE2025 Ni wakati muafaka sasa kwa WanaCCM kuonyesha nguvu yao kwa maslahi ya Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Benson Mramba

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2013
Posts
766
Reaction score
1,884
Kazi ya Chama cha CCM ni kuisimamia serikali yao itekeleze ilani yao ya uchaguzi.

Mpaka sasa naiona serikali yao ikituletea Xenophobia na nchi majirani zetu, vikwazo vya kiuchumi kutoka ulaya na marekani na mgawanyiko mkubwa ndani ya nchi kwa itikadi ya vyama kiasi cha kutishia amani na Umoja wetu kama Taifa.

Kwa maslahi ya Taifa ni muda wa wanaCCM sasa kuweka ushabiki pembeni na kuuvaa uzalendo halisi wa Chama na Taifa. Wana CCM wanapaswa kusikiliza kilio cha Wananchi na kufanya maamuzi magumu ya kulikomboa Taifa letu lisitumbukie korongoni.

Mbona wana CHADEMA waliweza kufanya mabadiliko kwa kusaidiwa na msukumo wa umma kupitia mitandao ya kijamii?

WanaCCM mkianza tu Umma utawasaidia. Askofu Gwajima ameanza muungeni mkono kwenye vikao vya chama. Muda hauko upande wenu. Taifa linawalilia na kuwategemea.

Wabillah Tawfiq
 
Kamanda hata siku Moja Spika haiwezi kuufunza Mdomo utamu wa CHAKULA.
 
Mkutano mkuu wa ccm mwisho wa mwezi huu ndio mwanzo mzuri wa anguko lao
 
Kazi ya Chama cha CCM ni kuisimamia serikali yao itekeleze ilani yao ya uchaguzi.

Mpaka sasa naiona serikali yao ikituletea Xenophobia na nchi majirani zetu, vikwazo vya kiuchumi kutoka ulaya na marekani na mgawanyiko mkubwa ndani ya nchi kwa itikadi ya vyama kiasi cha kutishia amani na Umoja wetu kama Taifa.

Kwa maslahi ya Taifa ni muda wa wanaCCM sasa kuweka ushabiki pembeni na kuuvaa uzalendo halisi wa Chama na Taifa. Wana CCM wanapaswa kusikiliza kilio cha Wananchi na kufanya maamuzi magumu ya kulikomboa Taifa letu lisitumbukie korongoni.

Mbona wana CHADEMA waliweza kufanya mabadiliko kwa kusaidiwa na msukumo wa umma kupitia mitandao ya kijamii?

WanaCCM mkianza tu Umma utawasaidia. Askofu Gwajima ameanza muungeni mkono kwenye vikao vya chama. Muda hauko upande wenu. Taifa linawalilia na kuwategemea.

Wabillah Tawfiq
Wana ccm wapi unawazungumzia?
 
Back
Top Bottom