Ni jambo lisilopingika kwamba samaki katika Ziwa Victoria wamepungua sana na inawezekana kwa asilimia 80. Kunusuru hali hii inabidi Serikali kupandikiza vifaranga wa samaki hasa wale wa sangari, dagaa, sato, mumi, ningu, kamongo, na wengineo kwa mamilioni ili idadi ya samaki iongezeke kwa kasi.
Sasa ni wakati muafaka Serikali kufunga uvuvi wa aina yeyote katika Ziwa Victoria hasa uapnde wa Tanzania kwa miezi sita ili samaki wapate kuongezeka kwa kasi. Kama itapendeza Serikali yetu ifanye mazungumzo na jirani zetu wa Kenya na Uganda kuhusu suala hili. Suala hili liwe la kisheria na matangazo yatolewe popote Kanda ya Ziwa na adhabu iwekwe kwa yeyote atakaye kaidi agizo hili. Baada ya miezi sita wavuvi watakuwa huru tena kuendelea na uvuvi kama mwanzo.
Nawasilisha.