Ni wakati muafaka serikali kufunga uvuvi wa samaki katika ziwa Victoria kwa muda wa miezi sita kuwezesha samaki kuzaliana

Ni wakati muafaka serikali kufunga uvuvi wa samaki katika ziwa Victoria kwa muda wa miezi sita kuwezesha samaki kuzaliana

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Ni jambo lisilopingika kwamba samaki katika Ziwa Victoria wamepungua sana na inawezekana kwa asilimia 80. Kunusuru hali hii inabidi Serikali kupandikiza vifaranga wa samaki hasa wale wa sangari, dagaa, sato, mumi, ningu, kamongo, na wengineo kwa mamilioni ili idadi ya samaki iongezeke kwa kasi.

Sasa ni wakati muafaka Serikali kufunga uvuvi wa aina yeyote katika Ziwa Victoria hasa uapnde wa Tanzania kwa miezi sita ili samaki wapate kuongezeka kwa kasi. Kama itapendeza Serikali yetu ifanye mazungumzo na jirani zetu wa Kenya na Uganda kuhusu suala hili. Suala hili liwe la kisheria na matangazo yatolewe popote Kanda ya Ziwa na adhabu iwekwe kwa yeyote atakaye kaidi agizo hili. Baada ya miezi sita wavuvi watakuwa huru tena kuendelea na uvuvi kama mwanzo.

Nawasilisha.
 
Tanzania tungefanya hivi,,tunafunga miezi 3,,na tuna ua miezi 9 Kila mwaka naamini samaki wangekuwa wengi.
 
Unapofunga ziwa ambalo ndio tegemeo la uchumi katika Kanda ya ziwa, maana yake unakaribisha umasikini Kwa eneo husika. Mtoa hoja yawezekana wewe sio mvuvi na kipato chako hakitegemei ziwa, pia yawezekana wewe ni muajiliwa. Ndio maana unatoa hoja nyepesi ambayo sio ya kiuchumi.
 
Ni jambo lisilopingika kwamba samaki katika Ziwa Victoria wamepungua sana na inawezekana kwa asilimia 80. Kunusuru hali hii inabidi Serikali kupandikiza vifaranga wa samaki hasa wale wa sangari, dagaa, sato, mumi, ningu, kamongo, na wengineo kwa mamilioni ili idadi ya samaki iongezeke kwa kasi.

Sasa ni wakati muafaka Serikali kufunga uvuvi wa aina yeyote katika Ziwa Victoria hasa uapnde wa Tanzania kwa miezi sita ili samaki wapate kuongezeka kwa kasi. Kama itapendeza Serikali yetu ifanye mazungumzo na jirani zetu wa Kenya na Uganda kuhusu suala hili. Suala hili liwe la kisheria na matangazo yatolewe popote Kanda ya Ziwa na adhabu iwekwe kwa yeyote atakaye kaidi agizo hili. Baada ya miezi sita wavuvi watakuwa huru tena kuendelea na uvuvi kama mwanzo.

Nawasilisha.
solution ni Kuanzisha mradi wa kuzalisha Vifaranga vya Sato mfano kwa Mwezi wanazalishwa vifaranga wa Sato 10 Millions na kumwagwa ziwani.....
View: https://www.youtube.com/watch?v=463QvdslCmQ&pp=ygUacGxhbmUgZHJvcHMgZmlzaCBpbnRvIGxha2U%3D Project itaicost Serikali kama dola million 4. ambayo wanaweza kukusanya kama ushuru kwa wavuvi/Wauza Samaki.
hili Tatizo sio Geni Duniani TAtizo nchi yetu wenye mamlaka awathink out of the box....Wanaweza yes kufunga ziwa for 3 mnth je wategemezi wa uvuvi lake zone watakula nini....................................Yes It can BE do Just Play your PArt-JK Nyerere
 
Naunga mkono hoja. Hili ziwa kama juhudi za makusudi hazitofanyika, litabakia na maji ya kunywa tu.
 
Wakifunga Tz majirani zetu Kenya na Ug watafunga pia?Au sisi ndio tutawanufaisha.
 
Nimesoma maoni yenu na mengine nimekubaliana nayo. Suala la kupandikiza vifaranga ni muhimu sana ili samaki wazaliane na kuwa wengi. Kufunga Ziwa ninaona ni jambo la muhimu angalau miezi mitatu na elimu itabidi itolewe kwa wavuvi kuwaonyesha faida watakayopata tukifunga Ziwa. Hali ya sasa ikiendelea katika Ziwa Victoria kwa miaka 10 samaki wote wataisha na ziwa litabaki kwa ajili ya maji ya kunywa na kumwagilia bustani kando kando ya ziwa.
 
Back
Top Bottom