Ni wakati muafaka wa kurudisha "BAKORA" mashuleni


Mkuu kwa hiyo kiboko,ndio njia pekee ya kuwadespline hao watoto?
 
ndo muda wake acheni vijana waenjoy ujana jemen, ka hvyo vboko vnaxaidia bax ata hao mafxad 2wachape kwa ku2ibia miela ye2 by th way kufeli skul xo kufel maisha...

ndo haya haya ma zero... X X X..
 
wote wanaoleta sera za kufuta mboko walicharazwa vya kutosha ndiyo maana wapo hapo, ni kweli kuna mambo mengi yaliyochangia kutufikisha hapa kama maslahi duni kwa walimu, wakidai wanapewa kebehi, kukosa umakini ktk training ya walimu, wengi wa walimu walio kazini ni wale waliopata alama za mwisho sekondari. Walimu haohao kwa kupigwa na inferiority, (kumbuka ajira hiyo kwao ilikuwa ni kimbilio la mwisho) hawawezi kudai maslahi yao kwa nguvu inayotakiwa (kama madaktari), hii imesababisha mgomo mkubwa kuendelea, na matokeo yake kila mtu anayaona.....
 
ka ujui uliza ujibiwe.. Lgha inakua na chngez ni invtabl hatupo kwnye enz zenu za 80's.!!! Nkikwambia pnts zang nlzozpata o.lvl utajidai xana kwa m2 ka mm kureply pst yko, ushazoea kuentract na vlaza wenzko...
rudi face book hapa hatuandikagi viswahili vya o-level
 
Mi nafsi yangu!

Nalaani alisemaga hakuna bakora shuleni.
Tena ingekuwa maamuzi yangu angestahili ashtakiwe mara moja yoyote yule alipokea huu mwongozo wa kuondoa bakora na ingestahili awaombe radhi Watanganyika.

Yani ametusogezea maradhi kabisa!

Naunga mkono hoja ya bakora kwa 100%!
 
Mkuu kwa hiyo kiboko,ndio njia pekee ya kuwadespline hao watoto?

kama umenisoma vizuri nimeshauri hatua hata zaidi ya viboko. Yaani wale wasio qualify kuwepo kwa nyanja yoyote iwe ya kitabia au uwezo wa ki masomo kutokana na standard za level aliyopo mtoto better aondoke. Mbaya zaidi viongozi wa siasa kama madiwani na watendaji wanaingilia hadi maamuzi ya ki professinal kiasi kwamba hata wakuu wa shule wanashindwa kuchukua hatua kwa kuogopa madiwani,kisa wapiga kura watakasilika.
 
mtoto ni mtoto tu kichapo lazma ukizingatia hawa wa siku hizi wanapevuka akiwa std 5 or 6,

Ndio tatizo,badala ya kuangalia kwa nini mtoto
anafeli mtu unakimbilia bakora.
Ndio maana wanafunzi wa vyuo wakiandamana
badala ya kutafuta chanzo serikali inakuja na
mabomu ya machozi.

Yanaanzia mbali haya.
 
Jamii yenyewe ilikuwa na maadili,haiwezekani jamii iliyopotoka ikawa na watoto wenye maadili.

Alivyo baba ndivyo alivyo mtoto,hata waweke mijeledi acha bakora,haita saidia.
 


Yawezekana uko thahihi ila ningependa nikukumbushe hivi mkuu kuiga tamaduni za magharibi iko siku tutalia coz ni sawa na kuiga step ya kucheza uciyoijua na mara tu utakapo gundua step ipasayo inakuwa too late.

Sawa seminary unazozisema mimi ckatai, lkn c ndo hizo zinazo tuzalishia viongozi waco na uzalendo na mafisadi coz hawazijui taabu na maisha halic ya mtanzania wa kawaida.

Kuhusu walimu na vitendea kazi vinginevyo ckubaliani na ww hata kidogo kwani nikikuunga mkono ni kuwalemaza watoto wetu. Kwa zamani tulisomaje? Mbona tulisoma kwa shida sana lkn tulikuwa tunafanya vizuri xana!

Viboko vilimlazimisha mwanafunzi kuxoma kwa bidii na kuwa na adabu ili kuepuka adha hiyo.

Hivyo viboko vina nafasi yake ktk maendeleo bora ya kinidhamu na kitaaluma kwa watoto wetu!
 
Nashangaa imagine mtoto wa kike ameshavunja ungo unamchapa??


Mkuu kuvunja ungo sio tija mimi mwenyewe niliadhibiwa Bakora nyingi nikiwa na ndevu nyingi kidato cha 6. Wanafunzi WAADHIBIWE TUOKOE TAIFA.
 
Ndio tatizo,badala ya kuangalia kwa nini mtoto anafeli mtu unakimbilia bakora. Ndio maana wanafunzi wa vyuo wakiandamana badala ya kutafuta chanzo serikali inakuja na mabomu ya machozi. Yanaanzia mbali haya.
lait ungejua kuondolewa viboko mashuleli kulivyofanya watoto wawe na dharau! Aisee japo wakwangu anasoma st nanii lakini nimewaomba walimu wamtandike pale anapofanya kosa linalostaili adhabu na mtoto anaadabu kiasi chake.
 
Mkuu kuvunja ungo sio tija mimi mwenyewe niliadhibiwa Bakora nyingi nikiwa na ndevu nyingi kidato cha 6. Wanafunzi WAADHIBIWE TUOKOE TAIFA.
Khaaaaaa!!! Mkuu Hiyo si sawa hata kidogo ila mwenyewe ulikuwa hujui kama si sawa,hapo hakuna tofauti na mjerumani alivyokuwa anampiga muafrika.

Ina maana katika umri huo form 6 na ndevu
zako ulikuwa hujajua tofauti kati ya baya na zuri??

Hata hivyo wengi waliolifikisha Taifa letu lilipo leo karibu wote ndio hao hao waliosoma kwa
viboko.
 
Uko sahihi Ikeli Nagiva. Swala la kutembeza viboko si suluhisho. Kuna sababu nyingi kwa nini mtahiniwa anaandika matusi au beti za bongo flava kwenye karatasi ya majibu. Kwanza ni kwamba hajui cha kuandika; kichwani mwake hana zaidi ya matusi na mashairi ya bongo fleva. Sababu ya pili ni maandalizi ya waalimu.Inatakiwa miezi miwili au mmoja kabla ya mtihani waalimu wafundishe kitu kinaitwa 'examination techniques' yaani mambo ya kufanya na kutofanya kwenye chumba cha mtihani. kwenye kipengele cha mambo ya kutofanya, waalimu wanatakiwa kueleza kuwa ni kosa kubwa kutoa majibu kwa swali lisiloulizwa. Haya yakifanywa kwa shule zenye waalimu pengine huu ujinga wa kuandika vitu vya ajabu kwenye karatasi za majibu utaisha au kupungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…