Black Legend
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 174
- 301
Ni muda mrefu sasa watumishi nchini wamekuwa wakinyimwa haki zao ambazo zingine ni za kikatiba kabisa, kwa mfano kupewa nyongeza ya mishahara kila mwaka (annual incriment), upandaji wa vyeo, ulipwaji wa madeni na stahiki zingine, n.k.
Kutokana uwepo wa vyama vya wafanyakazi (trade unions) kama TUCTA, TUGHE, TAU, CWT n.k, watumishi wamekuwa wanakatwa kiasi cha fedha kutoka katika mishahara yao kama michango ya uendeshaji wa vyama hivi.
Katika kipindi cha miaka 10/15 watumishi wamekuwa wakinyimwa haki zao za kiutumishi na pia kupewa ahadi zisizotekelezwa.
Uwepo wa vyama vya wafanyakazi ingekuwa ndiyo kimbilio lakini vyama hivi kwa sasa vimekuwa mzigo na kero kubwa kwa watumishi kutokana na kushindwa kuishi malengo ya matarajio ya kutetea haki za watumishi.
Ni wakati muafaka watumishi waombe kuangalia upya uwepo wa vyama hivi. Kama inawezekana sheria ifute ulazima wa kuwa mwanachama wa vyama hivi.
Mnakaribishwa kwa mjadala.