Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Hali ya Gaza inazidi kuwa mbaya na idadi ya vifo vinaongezeka kwani jeshi la Israel limekuwa huru kuua kama linavyopenda.
Wapiganaji wa Gaza wenyewe wametumia nguvu zao zote kujitetea mpaka wameishiwa nguvu.Hakuna cha kusifia kwa vikosi vya IDF kwani ni kama vile dunia nzima imeshirikiana na Israel kuwafunga mikono na miguu wapiganaji wa Gaza kuiachia Israel iwauwe.
Kilichotokea na kinachoendelea kutokea ni kuwa Netanyahu amewahadaa kikamilifu watu wa Gaza na kuwachokesha bure bila nafuu iliyotegemewa.Hatimae na Misri nayo ikaiwachia Israel ifunge mpaka wote na kudhibiti hata chakula kinachoingia Gaza.
Waziri wa Israel aitwaye Smotrich amesema sasa Israel ina uwezo wa kuwaua wapalestina wote waliobaki Gaza kwa njaa japo dunia anahofia huenda ikawazuia kufanya hivyo jambo ambalo pia hakuna nguvu ya kulizuia.
Nguvu na kasi ya Israel ya kupiga inapotaka na kuua kwenye maeneo yaliyotangazwa ni salama imekuwa kubwa sana.Hakuna tena kuchagua kambi ya wakimbizi au shule na hospitali. Inapiga tu kwa kutumia silaha nzito na kisingizio kinakuwa ni kumlenga kamanda wa Hamas.
Baada ya kuuliwa kwa Ismail Haniya Iran iliahidi kulipiza kisasi kwa kuipiga Israel. Hata hivyo raisi mpya wa Iran, Masoud amekuja na wazo la kutaka kuepusha vita hivyo yawezekana kwa woga au sababu nyengine za kiuchumi.
Tukirudi katika madhila yanayowakuta watu wa Gaza ambapo hakuna tena sehemu inayoitwa salama kuhamia na wameishiwa na nguvu. Ni wakati sahihi wa kupatikana nguvu kutoka nje itakayowaokoa kumalizwa kuuliwa na Israel.
Kwa vile maazimio ya UN na hukumu za mahakama hakuna hata moja iliyofanya kazi kuizuia Israel kuendelea kufanya unyama wake. Na kwa sababu hakuna taifa jengine lenye nguvu lililojitokeza kuleta nafuu.
Na kwa vile Iran pekee imejitokeza na ina sababu ya kuingia vitani na Israel, basi ni wakati munasibu kwa taifa hilo kumtegemea Mungu na kuingia kati kuwaokoa Wapalestina ili wasimalizwe kwa kuuliwa kwa silaha au kwa kunyimwa chakula.