Ni wakati sasa nafasi za watendaji zipatikane kwa ushindani

Tunaendelea

Rais katengua na kuteua mtu mwingine DART.

Tangu waanze kutenguliwa kumetokea ahueni gani?

Hoja yangu ni ile ile! Kama hatujagundua tatizo ni nini nchi hii kila siku tutakuwa tunapiga kelele tu na wala hatutatui matatizo yanayotukabiri.

Eti hadi Mkurugenzi wa DART anateuliwa na Rais alafu hao wateuliwa sasa hajui hata maana ya biashara!
 
Tuliwahi kuelekea kwenye hatua hiyo ya utendaji ya kutangaza nafasi na kuitisha usaili wa nafasi za kazi ambazo hazikuwa za kisiasa. Kilele cha utekelezaji kilikuwa wakati Mhe. Mkapa akiwa Rais. Pili, katika taratibu na kanuni za uteuzi na kupandishwa madaraja serikali, ubora na uwezo wa utendaji (merit) ndiyo vigezo vinavyotakiwa kutumika. Tatizo ni kwamba hata Kiongozi Mkuu anatakiwa awe wa vigezo hivyo ili aweze kutambua mantiki na faida kwa taifa ya kutumia hekima hiyo. Hapo ndipo wenzetu wa Zanzibar huita "Huo ni mtihani!" Basi tungoje siku ambayo tutafaulu tena huo mtihani.
 
Hoja yako ina mashiko sana Mkuu,safi sana!
 
Dawa ni katiba mpya, kupunguza mamlaka za uteuzi ili kuweka namna bora ya kupata watu wenye sifa..shida iliyo nayo Tanzania ni taasisi zinazofanya vetting..TISS wana matatizo makubwa!
 
Nashangaa sana.
Imefika hatua saivi Serikalini nasikia mtu anasoma masters ili tu apande cheo? Mambo ya ajabu kabisa. Badala ya kuangalia utendaji wa mtu na ufanisi wake katika kazi tunaangalia vitu vya ajabu eti masters. Ndo mana tumejaza masters na PhD ambazo hazitupi matokeo tunayohitaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…