Ni wakati sasa Nape Nnauye kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa

Mshajipima na kuona nafasi ya mwenyekiti nyepesi hivyo! nafuu aliyepita kuliko unayemtaka aje.
Unakumbuka Nape alivyokesha kuijenga CCM akiwa na kina Kinana enzi za CCM Goigoi zama za Kikwete?
 
Alitimiza wajibu wake , Hapo unamchimba Jk sasa.
Alipambana na mawaziri mizigo mpaka akachukiwa. Enzi za mwendazake alitolewa na kutishiwa bastola hadharani.

Nape anafaa kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa.
 
Alipambana na mawaziri mizigo mpaka akachukiwa. Enzi za mwendazake alitolewa na kutishiwa bastola hadharani!!
Kila Zama na Mambo yake, Ile bastola ilimfaa kwa kushiriki bao la mkono na ashukuru aliyemtolea alikuwa mgeni nayo.
 
Umeanza lini kuongelea habari za CCM? Kwani hujui katiba ya CCM inasemaje?
Au una mambo yako binafsi kichwani
 
Bangi unazovuta nakushauri uziache tu zinapokupeleka siko.
 
Jambo safi, Ila sio kwa Nape.

Wapo viongozi wazuri tu CCM wenye uwezo na busara kuongoza CCM kama chama. Nape sio mmoja wao.

Ukisema Nape agombee Uraisi sawa, halafu awepo Mwenyerungu aweze kumcharaza pale atapoanza kutuna tuna kama huko nyuma sawa kabisa.

Demokrasia ndani ya CCM ndie mwokozi wao.

Walifikirie hili Jambo.
 
CCM haina utamaduni huo, Mwenyekiti ni lazima awe Rais wa nchi. na Mwenyekiti hachaguliwi bali anaidhinishwa na wanachama.
Hii ndiyo tofauti kubwa iliyopo kati ya CCM na vyama vingine vya siasa.
 
Nimecheka sana kwa sauti!πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
kweli ccm itakuwa imekuwa mufilisi!πŸ€£πŸ˜‚
 
Una kichwa cha panzi! Unafikiri CCM ni utumbo utumbo kama mawazo yako!
Jipe nafasi ya kujifunza! Nape ni mwasiasa ndiyo lakini siyo wa kuwa Mwenyekiti wa CCM.
Una mtazamo wa kikomredi sana kwenye zama hizi ambako CCM kumejaa mabepari. Nape kwa sasa ndiye mwana CCM pekee anayeweza kuiongoza CCM.
 
Peleka ujinga wako huko. Mtu hata hajui mipaka ya madaraka yake? Alipokua waziri wa habari awamu ya tano kwa bifu lake kwa makonda kushikwa wema sepetu na bangi eti akaunda kamati kumchunguza makonda kuhusu kisa cha clauds, bila ya kutambua waziri hana madaraka kuunda kamati kama hiyo dhidi ya mkuu wa mkoa bila idhini ya rais. Pia kwa akili yake alifikiri kama waziri wa habari basi clouds ni issue yake bila kutambua mkuu wa mkoa ni mwakilishi wa rais mkoani na ana wajibu wa shughuli zote za serikali mkoana. Alivyohojiwa kuhusu wema alidai ana wajibu kumtetea kwa sababu mama zao wote wanatoka singida na eti baba zao wolikua marafiki.
Hapo sasa ndio ujue kwa nini magufuli akamtema wala si kwa sababu magufuli alikua mshamba.
Hebu kuweni serious jamani mnapopendekeza hawa wahuni kuchukua madaraka ya juu kwenye ccm au serikalini mnatushitua wengine.
 
Hebu kuweni serious jamani mnapopendekeza hawa wahuni kuchukua madaraka ya juu kwenye ccm au serikalini mnatushitua wengine.
Maelezo yako yanajipiga mtama yenyewe. Makonda hakuwa waziri. Lakini mpaka sasa ni Nape ndiye anatosha kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa. Nape anajua kutengeneza "Connections".
 
Naunga mkono hoja

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…