Kwa mlolongo wa kutoa huduma kwenye taasisi muhimu za serikali mfano ukienda NIDA kupata kitambulisho unachukua muda mrefu sana mpaka kupata namba ya NIDA na kitambulisho chenyewe unaweza usipate usipojiongeza vizuri.
Pia ukienda RITA kupata huduma tabu ipo palepale utazungushwa kwelikweli ila ukitoa rushwa unapata siku hiyo hiyo, pia ukienda kutafuta hati ya kusafiri(passport) inakuchukua muda mrefu na pia hii unaweza usipate kabisa kama haujiongezi.
Ukienda kwenye kupata leseni ya udereva nayo ni changamoto kupata hivyo hivyo, ila huduma zote hizo zinapatikana kupitia vishoka kwa njia za haraka kwa kutoa hela ili kufanikisha mchakato wako kwa haraka ndani ya siku moja, mbili au tatu unakuwa umeshapata huduma yako na kama umewapa hela nzuri vishoka unakuwa unapata huduma yako kwa haraka sana zaidi ya ulivyotarajia.
Sasa kukwepa hili ya hela kupotelea mikononi mwa watu wachache kwanini Serikali isiamue kuanzisha huduma ya haraka inakuwa ni V.i.P( express) ndani ya siku moja unakuwa umepata unachota kwa kulipia zaidi ili hii hela wanayochukua watumishi wasiowaaminifu ikaenda Serikalini.
Hata barabara za mwendokasi watu wangezilipia kupitisha magari yao ingekuwa na faida zaidi na kupunguza foleni zaidi kuliko watu wanavyopita sasa na kukamatwa ma mgambo wanaodai rushwa wanakuachiaaa
Note: huduma ya haraka iwe ni kwa wale waliokidhi vigezo vya kupatiwa huduma husika. Vitu vizuri ni gharama sana na wengi wanatamani kulipia kupunguza foleni na mchakato wa huduma.