Ni wakati sasa wa Gadiel na amekuchukua namba zao. Simba kocha aache kukariri

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Wakuu,

Ujue watu wamejiuliza sana kwanini wachezaji wazuri walipokuwa team zao kila wakienda Simba wanazikwa?

Gadiel wakati yupo yanga alimpokonya mpka Tshabalala namba national team alikuwa first choice na afcon alicheza mechi zote mpka wakati kuwania kwenda huko.

Lakini toka aje simba hapewi namba badala yake kishingo anampanga yule kilaza mtoto wake wa kambo tshabalala why? I think mechi na platinum gadiel aanze.

Tumeona tu kila anapopewa nafasi anam-prove wrong kishingo. Jana kafunga na goli. Sikumbuki Tshabalala lini kafunga.

Pia beki mzuri ibrahim ame hapati namba na badala yake yanapewa mazee kina wawa na onyango, yamechoka na yanakula pension za Burr kabisa.

Sasa sisi kama mashabiki wa simba tumechoka na uonevu huu wa kishingo kuua wachezaji.

Na pia Mwamedi hatumtaki. Katusajilia machezaji madudu matupu
 
I see..Gadiel tofauti na kupoteza pasi..kitu gani amefanya Jana?
 
Utopolo wenzako wako kimya ila wewe umeamua uandike utopolo.
 
Huu utopolo peleka kwa wachezaji wenu akina sarpong.

Unaongea hujielewi ni kama unatype ukiwa umevaa dera.
 
Gadiel foot work yake sio nzuri, ana drible apa mpira uko mita 7
 
hapana kwa kweli hapana hapaana,zimbwe yuko juu mno,ball contro kila kitu halafu hadi mwili wake siku hizi umeongezeka ila kuna kitu huwa nakiwaza sana hivi haiwezekani siku kocha akamuweka zimbwe namba tatu halafu gadiel kama namba 11?atasaidia kushambulia na kuja kukaba
 
Gadiel mwenyewe ni kama amekata tamaa hivi sijui amekumbwa na kitu ganii. Akiwa uwanjani siku hizi hachangamki kabisa anakuwa amezubaa zubaa tu nahisi benchi limeharibu saikolojia yake. Anakaba vizuri sana lakini hataki kubadilika na kujifunza namna nzuri ya kushambulia kutokea pembeni kwani siku hizi mabeki wanafanya kazi zote mbili kwa pamoja. Pia ajulishwe sio kila mpira anaopata lazima aupooze kwanza halafu anapiga "back pass" mingine akokote mwenyewe asogeze timu mbele. Ajifunze namna nzuri ya kupiga krosi za mwisho. Afanye sana mazoezi ya kulenga mashuti golini kwani mashuti yake yana nguvu lakini hayalengi goli kabisa. Akiyafanyia kazi hayo mapungufu yake kwa kweli atacheza kiwango cha juu na umri unamruhusu kucheza hata zaidi ya miaka 8 ijayo.
 
Mpuuzi ww, kuifunga majimaji ndio useme mchezaji mzuri, Gadiel hamfikii Zimbwe, sisi mashabiki wa Simba tunamkubali, ww baki na Utopolo yako.
 
Gadiel namfananisha na Emerson wa Chelsea alafu zimbwe na Alfonso davies wa Bayern munichen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…