Ni wakati sasa wa kumsaidia Amiri Jeshi Mkuu wetu

Ni wakati sasa wa kumsaidia Amiri Jeshi Mkuu wetu

Bhaghosha

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
234
Reaction score
183
Mheshimiwa Rais kapokea repoti ya CAG na kutoa hotuba kali iliyojaa uchungu na nchi yake.

Mheshimiwa Rais kaitoa hotuba mbele ya serikali yake, Lakini kikubwa mbele ya Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwa hotuba ile wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na mahakama wamepewa kazi ya kutekeleza mara moja.

Ninategemea kabisa, Mkuu wa majeshi ya ulinzi ataitisha kikao cha dharula cha wakuu wenzake ili kutafakari maagizo ya CinC wake na kutoa majukumu ya namna watakavyoyatekeleza.

Hawa mchwa wanaokula fedha ya wanainchi bila uchungu wanatakiwa kushughulikiwa mara moja bila huruma.

Kutokuwashughulikia ni sawa na kupinga amri halali ya mkuu wao na kutokutii kiapo chao cha utii kwa CinC, Nchi na usalama na haki za wanainchi.

Pia, ni wakati sasa vyombo vyetu viingilie kati, kwani wanasiasa na mhimili wa wabunge, washauri wa karibu wa raisi kikiwemo kitengo wameshindwa kutimiza wajibu wao kabisa. Zero.

Mungu ibariki na isaidie Tanzania, Mungu Mbariki na msaidie Rais wetu. Amen.
 
Kwa katiba tuliyonayo anaweza kufanya atakavyo aache kulialia na kutukana achukue hatua

USSR
 
Hizo mbwa ulizozitaja wanachoweza ni kumpiga risasi tundu na kumpachika kesi ya ugaidi mr free na kukamata wezi wa kuku hao wezi wa mabilioni ya taifa awawewezi sio saizi yao
 
Yeye ana instruments kibao. Ana ulinzi, ni consumer wa taarifa za kijasusi, atalipwa maslahi kibao hadi kufa kwake, sasa sisi tunaweza kumsaidia nini ambacho hakiwezi?
 
Kwanza ni CAG na sio CIG.... Halafu mama hajatoa muongozo wowote kuhusu hatua gan zichukuliwe kwa wale watu.

Kwa hyo waache watu wale kwa urefu wa kamba yao, kama mama alivyosema
 
Wizi haujaanza leo, aache huruma, hata kama umezaliwa kwenye maadili ya aina gani huwezi kuwanyamazia majizi

Aamue tu kwani ulinzi anao na wasaidizi kama hawansaidii basi ajue yeye ndio hawamtaki ili waendelee kuiba

Mtu anaiba $50m kirahisi hivyo
Watu wameiba tangu Enzi za mwalimu wengine mpaka sasa bado wanaishi na kuendeleza wizi mpaka watoto na wajukuu pia wanaiba tu

Hivi kweli kiongozi usingizi unapita kabisa kwa kuwaona watoto wanaambiwa waje na majivu shuleni huku ameiba mabilioni

Basi hata kuwasaidia hao watoto kwa kuwapa msaada
Mlaaniwe nyie majizi mpaka vitukuu vyenu
Mnaiba mpaka vya kwenu
Pm kama hana meno basi yuko nao
 
Kwani yeye si ndo Amiri jeshi mkuu, anakwama wapi???
 
Back
Top Bottom