Ni wakati wa Ali Kiba

Ni wakati wa Ali Kiba

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kamwe tusimdharau Diamond... Ana mafanikio kuanzia cash, umaarufu, kutoa ajira kuitangaza nchi kimuziki nknk... Amepata nafasi na akaitumia vema... Ni bahati na fursa ya kipekee sana aliyotunukiwa... Atakumbukwa na vizazi vingi..
Juu ya yote hayo kila kizuri hakikosi kasoro.... Huwezi kufanikiwa kwenye kila kitu lazima kuna mahali utafeli... Diamond kwenye mahusiano kafeli.. Na hiki ndio kinaweza kuwa kiama chake... Fimbo ngumu ya kumwadhibu!

Lakini je Diamond ni wa kulaumiwa? Ni wa kuchekwa? Ni wa kunyooshewa vidole kila kona? La hasha labda tu kama wewe ni mpenda umbea... Una roho ya kwanini... Na ni mtu mwenye husuda...
Kiroho matendo ya sasa ya Diamond kwenye mahusiano yana asili na huko alikotoka na mahusiano yake rasmi ya kwanza....

Diamond kalelewa na mzazi mmoja (mama) baba yake mzazi ni aina ya wale wazazi katili wanaojua kutundika mimba tu lakini malezi kwa mama... Hili roho linamuandama Diamond
Mpenzi wake wa kwanza kujulikana na wote Wema Sepetu ana historia karibu sawa na Diamond.... Wote hawa inawezekana kabisa kwa sehemu kubwa ya maisha yao hawakufurahia ama hawana uzoefu na malezi ya FAMILIA iliyosimama yenye baba na mama nk... Wana common sharing... Hili pia ni tatizo....
Mpaka sasa si Wema wala si Diamond hakuna mwenye ramani inayoeleweka kwenye mahusiano... Kwahiyo kwa diamond hiki ndio kinaweza kuwa TAMATI ya kilele chake cha mafanikio... Habari za...
.kutengana na mzazi mwenzake
. habari za kuzaa nje ya mahusiano
. habari za kuitwa kwenye vyombo vya usuluhishi
. habari za kufunguliwa mashtaka
. habari za kuitwa polisi...... Si mambo yanayowekwa kwenye kundi la mafanikio bali mwanzo wa anguko ama tamati ya kilele cha mafanikio

Ni wakati wa Ali Kiba sasa
Ni mmojawapo wa wasanii wenye vipaji alianza vizuri lakini kuna wakati akarudi nyuma inasemekana alikuwa Tanga.. Sijui wanawake wa Tanga walimfanya nini huko... Kidogo tumpoteze...

Waswahili wanasema kosea vyote lakini sio kuoa.. Kiba tangu arudi hewani ameendelea kufanya vizuri... Sasa kaingia kwenye ndoa. Ndoa hii iwe ni mwanzo wa mafanikio na isiwe ndio mwanzo wa kumpoteza mazima.... Yupo wapi Marlaw
Sanaa na ndoa inahitaji balance ya hali ya juu sana.. Mwenza akishakua negative... Anguko haliko mbali...
Ni wakati wa kiba sasa lakini kama tu kapata mtu sahihi mwenye akili ya kujua kuwa sanaa ya mumewe ndio bright future yao...
 
Maandalizi ya ukumbi itakapofanyika hafla ya harusi ya Kiba... Huku itakuwa ni suit kali na shella hakuna majambia View attachment 760669View attachment 760671
IMG-20180429-WA0089.jpg
 
Kama sio wa kwanza kucomment basi nahisi sio wa tatu[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji377] [emoji377] [emoji377] [emoji124] [emoji125] [emoji125]
 
Nakubaliana na wewe!
Diamond ametoa album lakini mtaani wala hakuna zile amsha amsha kama zamani hata akisema tarehe flani anachia ngoma mtaa mzima kimya!!

Hata ukisikiliza hupati ile radha tamu iliyokuwepo zamani kwenye nyimbo zake
 
Kila nikimtizama Diamond ana miaka kama mi3 au mi4 ya kuendelea kufanya vizuri, yy mwenyewe anajiona kama underground na ndio maana kila siku anafanya vitu vipya vikubwa,mwaka jana kaalikwa mataifa huru ya Africa mwaka huu World Cup Russia hatujui mwakani ataalikwa wapi,bado hapo ana bidhaa kibao ameziingiza sokoni na zinafanya vizuri (Wasafi label &Record,Karanga,Wasafi TV&Radio,Perfume).Msanii pekee alifanikiwa KUINTERGRATE MZIKI WAKE NA BIASHARA, na ndio maana ana beef na washikadau wengi sababu wao wanapenda kuendesha mambo KISHIKAJI (hii ndio sababu wasanii wengi wanakuwa masikini) na si KIBIASHARA kama yy anavyotaka.
 
Nakubaliana na wewe!
Diamond ametoa album lakini mtaani wala hakuna zile amsha amsha kama zamani hata akisema tarehe flani anachia ngoma mtaa mzima kimya!!

Hata ukisikiliza hupati ile radha tamu iliyokuwepo zamani kwenye nyimbo zake

Kama haya ni ya kweli nitaamini kuna mafanikio ya kishirikina! I am watching and learning!
 
Nakubaliana na wewe!
Diamond ametoa album lakini mtaani wala hakuna zile amsha amsha kama zamani hata akisema tarehe flani anachia ngoma mtaa mzima kimya!!

Hata ukisikiliza hupati ile radha tamu iliyokuwepo zamani kwenye nyimbo zake
Ukitaka kujua hiyo album imetapakaa ,nenda kariakoo watu wanaiuza kama njugu.Juzi nilikuwa natoka shamba kibaha madereva waboda boda wanazipiga zile nyimbo huko youtube usiseme kwa muda wa mwezi 1+ ,nyimbo yake ya Africa beauty ina jumla ya viewers milion 11+ na bado ktk album yake kuna nyimbo inaitwa Iyena ukitaka kujua ukubwa wa nyimbo hii nenda kwenye vigodoro,lazima ipigwe.
 
Kama haya ni ya kweli nitaamini kuna mafanikio ya kishirikina! I am watching and learning!
Kiukweli nilikua mpenzi sana wa muziki wake ila kwasasa nimeshindwa mkuu!
Labda tatizo lipo kwangu tu
 
Ukitaka kujua hiyo album imetapakaa ,nenda kariakoo watu wanaiuza kama njugu.Juzi nilikuwa natoka shamba kibaha madereva waboda boda wanazipiga zile nyimbo huko youtube usiseme kwa muda wa mwezi 1+ ,nyimbo yake ya Africa beauty ina jumla ya viewers milion 11+ na bado ktk album yake kuna nyimbo inaitwa Iyena ukitaka kujua ukubwa wa nyimbo hii nenda kwenye vigodoro,lazima ipigwe.
Itakua tatizo lipo kwangu mkuu!
Kiukweli siipati ile radha niliyokua naipata zamani kwenye ngoma zake!
 
Itakua tatizo lipo kwangu mkuu!
Kiukweli siipati ile radha niliyokua naipata zamani kwenye ngoma zake!
Labda kwako ila jamaa yupo vizuri,ila tatizo washika dau wanataka kumshusha ila raia mtaani wanamsikiliza sana.Ujue nimekuja kugundua kuna wasani wanapata air time sana kwenye maredio na wale wanaopata airtime uswahilini,ila kwa wasanii wenye airtime kubwa hasa uswahilini ni Aslay,Diamond,Rayvany na Harmonize mpaka hivi sasa.
 
Diamond ni vigumu kupotea, ni mtu anayeelewa kazi yake, kipi akifanye na kwa mda gani, kukubalika kwa diamond haujawahi kuwa kwa sababu ya maisha yake binafsi bali kazi zake, ni kijana mbunifu sana ukilinganisha na vijana wengi walioko kwenye Sana'a.
Ushauri wangu kwake, anatakiwa kuwa na maisha bora kidogo nje ya Sana'a, hasa familia.
I support all of them, I would have loved their life to be a success.
 
Natazama tu,ila najua watakao ingia ni washamba washamba fulani hivi na haitobamba kama ile ya joti.
Vijanawalio karibu na akina KIBA hawajulikani yaani hawana ushawishi mjini.

Kifupi itakuwa ya kidwazi sana.
 
Huyu kijana alijisahau sana.
Aliishia kutongoza kuzalisha kuacha sasa acha ale matapishi yake
Hakuna kitu kibaya kama kuyaweka maisha yako kwenye social media
Anavuna alichopanda
Naona na tununu naye yupo busy na social media ataangukia pua siku si nyingi then itakuwa historia na hadithi njoo utamu kolea
Wasanii wa bongo wanajidanganya na neno 'celebrity' hahahhhhhhh watembelee Beverly Hills ndio wataelewa maana ya kuwa celebrity
Wao ni kutongozana kubadilishana kuachana kuzalishana what a big mess
Ali Kiba yupo humble down to earth anasonga
All the best Ali Kiba maisha mema ya ndoa umeamua vyema Mungu awajalie mema!
 
Back
Top Bottom