Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kamwe tusimdharau Diamond... Ana mafanikio kuanzia cash, umaarufu, kutoa ajira kuitangaza nchi kimuziki nknk... Amepata nafasi na akaitumia vema... Ni bahati na fursa ya kipekee sana aliyotunukiwa... Atakumbukwa na vizazi vingi..
Juu ya yote hayo kila kizuri hakikosi kasoro.... Huwezi kufanikiwa kwenye kila kitu lazima kuna mahali utafeli... Diamond kwenye mahusiano kafeli.. Na hiki ndio kinaweza kuwa kiama chake... Fimbo ngumu ya kumwadhibu!
Lakini je Diamond ni wa kulaumiwa? Ni wa kuchekwa? Ni wa kunyooshewa vidole kila kona? La hasha labda tu kama wewe ni mpenda umbea... Una roho ya kwanini... Na ni mtu mwenye husuda...
Kiroho matendo ya sasa ya Diamond kwenye mahusiano yana asili na huko alikotoka na mahusiano yake rasmi ya kwanza....
Diamond kalelewa na mzazi mmoja (mama) baba yake mzazi ni aina ya wale wazazi katili wanaojua kutundika mimba tu lakini malezi kwa mama... Hili roho linamuandama Diamond
Mpenzi wake wa kwanza kujulikana na wote Wema Sepetu ana historia karibu sawa na Diamond.... Wote hawa inawezekana kabisa kwa sehemu kubwa ya maisha yao hawakufurahia ama hawana uzoefu na malezi ya FAMILIA iliyosimama yenye baba na mama nk... Wana common sharing... Hili pia ni tatizo....
Mpaka sasa si Wema wala si Diamond hakuna mwenye ramani inayoeleweka kwenye mahusiano... Kwahiyo kwa diamond hiki ndio kinaweza kuwa TAMATI ya kilele chake cha mafanikio... Habari za...
.kutengana na mzazi mwenzake
. habari za kuzaa nje ya mahusiano
. habari za kuitwa kwenye vyombo vya usuluhishi
. habari za kufunguliwa mashtaka
. habari za kuitwa polisi...... Si mambo yanayowekwa kwenye kundi la mafanikio bali mwanzo wa anguko ama tamati ya kilele cha mafanikio
Ni wakati wa Ali Kiba sasa
Ni mmojawapo wa wasanii wenye vipaji alianza vizuri lakini kuna wakati akarudi nyuma inasemekana alikuwa Tanga.. Sijui wanawake wa Tanga walimfanya nini huko... Kidogo tumpoteze...
Waswahili wanasema kosea vyote lakini sio kuoa.. Kiba tangu arudi hewani ameendelea kufanya vizuri... Sasa kaingia kwenye ndoa. Ndoa hii iwe ni mwanzo wa mafanikio na isiwe ndio mwanzo wa kumpoteza mazima.... Yupo wapi Marlaw
Sanaa na ndoa inahitaji balance ya hali ya juu sana.. Mwenza akishakua negative... Anguko haliko mbali...
Ni wakati wa kiba sasa lakini kama tu kapata mtu sahihi mwenye akili ya kujua kuwa sanaa ya mumewe ndio bright future yao...