Ni wakati wa machinga, mama ntilie na wafanyabiashara wadogo kulipa Kodi halali

Woga tupa kulee

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2012
Posts
1,752
Reaction score
1,311
Najua wapo watakao sema ni ukatili, hapana.

Kama ambavyo wafanyakazi wanao lipwa sh hata laki nne kwa mwezi hukatwa Kodi kila mwezi, ni wakati wa wafanyabiashara tajwa kulipa Kodi halali itakayo kusanywa na TRA, sio hivyo vitambulisho vya 20,000 ambayo hatujawahi kuambiwa huwa inakwenda wapi!!

Mmachinga mwenye mtaji wa shilingi laki tano, kwa siku huzalisha faida ya hadi shilingi elfu kumi baada ya kutoa chakula na gharama zingine za maisha, huyu kwa mwezi anazalisha sh laki tatu na kwa mwaka sh milioni tatu na ushee.

Wawekewe Kodi hata flat rate ya elfu themanini kwa mwaka itakayo lipwa kwa awamu nne. Hii kwa idadi ya wamachinga na wafanyabiashara wadogo waliopo itaongeza Kodi kwa mabilioni kwa serikali itakayo wawezesha kuhudumiwa vyema zaidi na serikali.

Binafsi wazazi wangu ni wafanyabiashara wadogo na hivyo nisichukuliwe kama nawachukia. Tulipe Kodi halali kwa maendeleo yetu.

Kazi iendelee
 
Mnashindwa kuwaza miradi mikubwa mnataka kodi za wauza maandazi. Kweli?

Aliyeturoga alikufa.
 
Hizo kodi za wauza maandazi zinatosha kuenendesha nchi?

Look into the bigger picture.

Hatuwezi kuendelea kwa mawazo haya.
 
Umewasahau na bodaboda! Hawa wapuuzi hawalipi kabisa kodi! na wakati kwa siku wana uwezo wa kuingiza mpaka elfu 50 na kuendelea!

Kutokana na kuachwa kwao kulipa kodi! Wamejikuta wanaishia tu kuzichezea hela wanazo pata na kugeuka tu kuwa kero kwa raia wengine kwa kujihusisha na ukwapuaji wa mikoba ya akina mama mjini, kufanya uzinzi na wake za watu, kuwajaza mimba wanafunzi.

Kuchezea fedha wanazopata kwenye michezo ya kubashiri na yale makorokocho ya Wachina! Wangekuwa wanalipa kodi hawa viumbe, sidhani kama wangepata hata muda wa kunyoa Viduku na kutupigia honi hovyo hovyo njiani tutembeapo kwa miguu.
 
Mtu mwenye turnover ya 10,000 kwa siku ni NIL Mkuu.
 
Hizo kodi za wauza maandazi zinatosha kuenendesha nchi?

Look into the bigger picture.

Hatuwezi kuendelea kwa mawazo haya.
Kila mtu alipe kodi kulingana na uwezo wake. Mimi hapa kila mwezi nakatwa laki 2 na 30 hivi kama kodi! Kwa mwaka nalipa kiasi gani?

Walipe hata elfu 10 tu kwa mwezi. Ili nchi iendelee, inatakiwa kila mwenye sifa ya kulipa kodi, alipe! Hakuna cha mnyonge wala nani. Kama anastahili kulipa, alipe ili Nchi iendelee.
 
Kisheria, mtu mwenye kipato(Net Profit) cha chini ya Milioni nne kwa mwaka hatakiwi kulipa kodi.
Acha uongo wako, nenda TRA uwaambie una kipato cha chini ya million 4 uone kama hautakadiriwa kodi.
 
Kabisa. Yaani ku widen tax base Ni kuongeza inclusion katika walipaji wa Kodi. Serikali ishughulikie hili.
 
Kwakweli hii sekta ya Wamachinga ndio inayolisha na kupeleka Watanzania wengi Mashuleni baada ya Wakulima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…