Woga tupa kulee
JF-Expert Member
- Sep 4, 2012
- 1,752
- 1,311
Najua wapo watakao sema ni ukatili, hapana.
Kama ambavyo wafanyakazi wanao lipwa sh hata laki nne kwa mwezi hukatwa Kodi kila mwezi, ni wakati wa wafanyabiashara tajwa kulipa Kodi halali itakayo kusanywa na TRA, sio hivyo vitambulisho vya 20,000 ambayo hatujawahi kuambiwa huwa inakwenda wapi!!
Mmachinga mwenye mtaji wa shilingi laki tano, kwa siku huzalisha faida ya hadi shilingi elfu kumi baada ya kutoa chakula na gharama zingine za maisha, huyu kwa mwezi anazalisha sh laki tatu na kwa mwaka sh milioni tatu na ushee.
Wawekewe Kodi hata flat rate ya elfu themanini kwa mwaka itakayo lipwa kwa awamu nne. Hii kwa idadi ya wamachinga na wafanyabiashara wadogo waliopo itaongeza Kodi kwa mabilioni kwa serikali itakayo wawezesha kuhudumiwa vyema zaidi na serikali.
Binafsi wazazi wangu ni wafanyabiashara wadogo na hivyo nisichukuliwe kama nawachukia. Tulipe Kodi halali kwa maendeleo yetu.
Kazi iendelee