Ni wakati wa Mourinho kumpanga Mkhytarian kama Namba 10

Ni wakati wa Mourinho kumpanga Mkhytarian kama Namba 10

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Huyu jamaa ni fundi wa mpira sana, ana ujuzi wote wa kucheza namba 10 yaani nyuma ya Straika. Ana piga pasi za mwisho, mwepesi, ananyumbulika na ni mtulivu hana papara na pia anarekodi nzuri ya kufunga magoli. Kuendelea kumcheza kwenye winga ya kulia ni kupoteza kipaji chake.

Wakati umefika sasa wa Mourinho kuachana na Pogba kama namba 10 na kuanza kumtumia ipasavyo Henrik Mkhytarian kama namba 10 kwa manufaa ya timu. Pogba arudi kwenye jukumu la Kiungo wa kati ambapo nguvu zake zitatumika vyema na sio namba 10 ambapo anaonekana wazi amekosa utulivu.

Kwa kumalizia:
Mou pia aache uoga wa kumuweka benchi Lingard. Dogo Lingard ana nini spesho cha kumuweka nje Martial? Ni wakati wa kumpa muda wa kutosha Martial nae aonyeshe uwezo wake.

Ni mtazamo tu.
 
Miki ni mchezaji anaejua kutoa mpira kwa wakati jamaa ni fundi sana
Ila nashangaa jinsi Mou anavyoua kipaji cha jamaa. Siku atakayoshtuka kumpanga jamaa kati itakuwa ni too late.
 
mchochezi ni kweli hello kwamba namba kumi inabidi awe mwepesi kuliko hata tisa nafikiri mou anampanga huyu paulo kwa sababu ameletwa na pesa nyingi halafu anawaza herera kumweka nje ni hasara
 
Last week wakati wanacheza na Liverpool si alimpanga hapo nyuma ya main striker? Dogo wa kawaida tu. Anyway, hizi "kelele" za kutaka kuonyesha Mourinho hajui afanyalo naona zimeanza baada ya draws na vipigo. EPL tamu sana. Na bado.
 
Morinho anachotaka ni hela tu , anunue january avunje rekodi ya PSG , Kocha anapenda sifa utadhani mkazi wa Kigogo Sambusa !
 
Back
Top Bottom