SoC02 Ni wakati wa taifa kuhakikisha ukuaji wa uchumi unaendana na hali halisi ya maisha ya watanzania

SoC02 Ni wakati wa taifa kuhakikisha ukuaji wa uchumi unaendana na hali halisi ya maisha ya watanzania

Stories of Change - 2022 Competition

SIMBA - X

Member
Joined
Aug 8, 2022
Posts
25
Reaction score
12
Utangulizi
Uchumi, kwa maana fupi ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa. Tanzania inakadiriwa kuwa uchumi wake kwa mwaka 2022 utaongezeka hadi kufikia asilimia 5.5 % kutoka 4.9% ya mwaka 2021, kulingana na makadirio kutoka benki kuu ya dunia. " worldbank.org" (Tovuti ya benki kuu ya dunia WB).

Kwa muujibu wa serikali, Kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2021/22 kulitokana na uwekezaji wa kimkakati hususani katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu, ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege, na kuongezeka kwa mikopo katika sekta binafsi ambayo imechochea shughuli za kiuchumi. (Rejea NBS 2021).

Katika andiko hili, nitazungumzia kuhusu utofauti baina ya takwimu za kukua kwa uchumi wa taifa na hali halisi ya maisha ilivyo hivi sasa ya kila mtanzania.

Kwa uhalisia hali ya mtanzania ilivyo hivi sasa, imezidi kuwa duni ambapo tukimuuliza mtanzania mmoja mmoja, hapa lazima atakujibu kuwa hali ya uchumi ni mbaya kwenye Elimu, Siasa, kilimo, ajira, uvuvi, afya, nishati ambapo tukilinganisha na takwimu za serikali kuhusu Tanzania kukua kwa uchumi ni wazi kumekuwa na utofauti.

Mfano halisi ni kuongezeka kwa deni la taifa, "hadi Aprili 2022 deni lilikuwa shilingi trilioni 69.44 ikilinganishwa na shilingi trilioni 60.72 kipindi kama hicho mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 14.4% ambapo kati ya kiasi hicho deni la nje lilikuwa shilingi trilioni 47.07 na deni la ndani lilikuwa shilingi trilioni 22.37" (Nukuu kutoka bungeni kwenye hotuba ya waziri wa fedha na mipango Dr. Mwigulu nchemba 2022).

Tukiangalia hapo kwenye deni la mwaka 2022 tunaona limeongezeka hadi shillingi trioni 69.44 kutoka shilingi trioni 60.72 ya mwaka jana 2021, inamaana deni la taifa kwa mwaka mmoja ambalo limeongezeka ni zaidi ya shilingi trioni 8.72 ambapo tukiangalia na Maeneo mengi ya watanzania mpaka sasa bado yakiwa hayana huduma za maji, madaraja, madarasa, huduma za afya, ambapo tukilinganisha na takwimu ya serikali kuhusu kukua kwa uchumi wa taifa kunaleta utofauti iweje uchumi ukue bila maendeleo ya taifa kuonekana kwa watanzania.

Katika uhalisia, ni wazi kwamba takwimu za kukua kwa uchumi haziendani na hali halisi iliyopo ya kila mtanzania, kumbuka mwaka 2020 Tanzania tulitangaziwa nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati kwa asilimia 4.8%, inamaana kwamba uchumi uliongezeka mara dufu kuja mwaka 2021 na 2022 hadi kufikia asilimia 5.5% ambapo tukiangalia hali halisi ya watanzania ni kwamba kuna wafanyakazi mpaka leo hii bado hawana nyongeza za mishara na wakati tunatangaziwa uchumi wa taifa umekua, (TUCTA 2022).

Kwenye upande mwengine wa kodi, tukiangalia hali halisi ya mtanzania kwenye vipato wanavyo pata ni vidogo sana. kodi zimezidi vipato vya watanzania kwa mfano halisi, ni kwa mtanzania mwenye mshahara mdogo wa chini kabisa. ambapo anapolipwa mshahara anatozwa kodi, akienda kutoa mshahara anatozwa kodi na akinunua kitu anatozwa kodi. kwahiyo kama mshahara wake ulikuwa ni elfu 20, inamaana jumla ya mshahara wake wote unaishia kwenye makato ya kutozwa kodi. Kumbuka hapo kuna wengine wanafamilia zinawategemea na bado mshahara hautoshi. Lakini pia Kwenye upande wa vifurushi vya mitandao, vimezidi kupanda bei pamoja na ongezeko la tozo za miamala ambazo zimesababisha mkanganyiko kwenye takwimu za ukuaji wa uchumi katika taifa.

Katika upande wa ajira, kuna wahitimu na wasomi wengi sana wapo tu mitaani wao wamesoma na wana vyeti vyao lakini hawana ajira. Vilio vya watanzania vimekuwa ni vingi wakati tunaambiwa uchumi umepanda na kuongezeka hadi asilimia 5.5% hali imekuwa ni mbaya kwa mfano kwa wale watanzania walioamua kujiajiri wamachinga, kumekuwa na majanga na matukio ya moto kila kukicha kwenye biashara za maeneo ya wamachinga tu, matukio ya moto yamezidi kuongezeka na kusababisha hasara Kwa watanzania vilio vimekuwa ni vingi na umaskini umezidi kuongezeka. FB_IMG_16613535947121290.jpgFB_IMG_16613536228515876.jpgFB_IMG_16613538405185944.jpg
(Picha kutoka mtandaoni).

Kwenye upande wa afya, hali imekuwa ni mbaya Sana kwenye vituo vya afya kumekuwa na upungufu wa wataalamu wa afya, uhaba wa vifaa, upungufu wa madawa, pamoja na huduma mbovu za matibabu kwa wagonjwa ambazo zimesababisha watanzania kuteseka. Tukiangalia Kwenye upande wa elimu, kumekuwa na mitaala mibovu ya kufundishia na kuna wanafunzi mpaka sasa hawana madarasa, madawati na wengi wao wanasomea chini ya mikorosho na wengine kwenye mabanda. vifaa vya kufundishia mashuleni hakuna na wanafunzi wengi hawana huduma za choo, sare za shule, vitabu vya kujifunzia, madaftari, peni, rula, maabara ya kufundishia masomo ya sayansi wakati tuna tangaziwa uchumi wa taifa umekua.

Mapendekezo
• Serikali iweke mfumo maalum utakao weza kuboresha Huduma za afya. kwasababu kumekuwa na mapungufu kwenye Huduma za afya mfano kwenye hosptali ya muhimbili kumekuwa na foleni kubwa kiasi kwamba wagonjwa wengine walio zidiwa wana panga foleni kwaajili ya matibabu hata masaa mawili, kwahiyo serikali iboreshe huduma za afya ili ukuaji wa uchumi uendane na hali halisi ya maisha ya watanzania.

• Serikali iwaongezee wafanyakazi mishahara ili ukuaji wa uchumi uendane na hali halisi ya watanzania. pengine nyongeza za mishahara kwa wafanyakazi inaweza kuwa fursa kwa wasio kuwa na ajira. kwamba wafanyakazi wakiongezewa mishahara watapata nafasi ya kujikwamua kiuchumi kwa kufungua biashara zao, ambapo inaweza kupelekea kuajiri wale wasio na ajira kupata kazi na kupunguza idadi ya tatizo la ajira ambapo itafanya ukuaji wa uchumi uendane na hali ya maisha ya watanzania.

• Serikali iweke kiwango maalum cha kodi ambacho kitaendana na hali halisi ya watanzania. Kutokana na kiwango kikubwa cha kodi kumesababisha watanzania kushindwa kuendesha maisha yao, kwasababu kodi zimezidi viwango vya mapato ya watanzania, hivyo inapaswa kuangaliwa kiwango chengine ambacho kitawawezesha watanzania kupata nafasi ya kujikwamua kiuchumi.

• Serikali iboreshe mitaala ya elimu ili ukuaji wa uchumi ulingane na hali halisi ya watanzania. Kwamba mitaala ya elimu iliyopo na ukuaji wa uchumi haviendani mfano tukiangalia kwenye upande wa sayansi na teknolojia, mitaala dhaifu ya elimu imesababisha kuwa na wataalamu walio na viwango ambavyo haviwezi kuleta ushindani na mataifa ya nje.

• Serikali ianzishe utaratibu maalum wakuwawezesha kwanza kiuchumi wafanyabiashara wadogo wadogo wamamchinga ili ukuaji wa uchumi uendane na hali halisi ya watanzania. Kumekuwa na matukio ya moto kwa wafanyabiashara wadogo, ambapo ukilinganisha ni kwamba watanzania wengi tunategemea kufanya ununuzi wa mahitaji ya bei nafuu kwa wamachinga, kwa hali ya matukio ya moto imeathiri sehemu kubwa ya watanzania. Kwahiyo ni wazi kwamba wafanyabiashara wadogo wanahitaji sana msaada wa kuwawezesha kwenye upande wa kuwaboreshea biashara zao hususani kwenye masuala ya ulinzi ili ukuaji wa uchumi uendane na watanzania.

Hitimisho
Taifa linatakiwa kufanyiwa mabadiliko makubwa ili liweze kuendelea mbele kiuchumi, kwasababu tunahitaji maendeleo mazuri itabidi tujitoe kufanya malekebisho pale ambapo pana mapungu tupalekebishe . tunachotakiwa ni kufanya mabadiliko na uwazi ili tupate nafasi ya kuangalia wapi tulipo kosea alafu tupalekebishe ndipo taifa litakuwa linaendelea kiuchumi.


 
Upvote 5
Karibuni kwa kuchangia mitazamo chanya kwenye chapisho hili.
 
Back
Top Bottom