Ni wakati wa watumiaji wa injini za boti ndogo kugeukia injini za kichina

Ni wakati wa watumiaji wa injini za boti ndogo kugeukia injini za kichina

Ni wakati sahihi kwa watumiaji wa injini za boti kwa ajili ya uvuvi, utalii na matumizi binafsi kugeukia injini za kutoka China baada ya miaka mingi kutumia injini zenye brand kubwa kama Yamaha, Suzuki, Mercury, Honda, Envirude, Tohatsu na Torpedo.

China sasa wamekuwa wakitengeneza injini za boti kama Parsun na Calon Grolia.

Sasa kwenye uvuvi kumiliki injini ya boti imekuwa ni jambo kubwa na gharama za ununuaji zipo juu. Tukigeukia injini za China bei ni ya kawaida na zina utumiaji mzuri wa mafuta. Spea zake zipo na bei si ghali sana.

View attachment 1486730

View attachment 1486732
Ungeweka makadirio ya bei ukute zinapishana laki 5 tu
 
Harafu injini ya kichina ina maisha mara nne chini ya urefu wa maisha ya yamaha. Yamaha inagonga miaka 10 kazini mchina miaka miwili tu ina hali mbaya kichizi. Mchina kumwondoa majini yamaha bado sana kwa hali hii niionayo ziwa nyanza
 
Mkuuu wambie.
Karibu sana Mabhibhi Mkuu. Ukiwa na Mchina wako nakupita na Yamaya yangu kama umesimama vile
 
Back
Top Bottom