Wakuu nazimia sana aina hii ya nyumba kwani zipo very simple,attractive,compact na zinakula nafasi ndogo sana.
Ni wapi kwa Dar wanatoa huduma ya ujenzi wa aina hii ya nyumba na gharama huwa ni sh ngapi?
Hizi nyumba huwa zinanivutia sana hasa kwenye design yake ilivyo,imagine haka hapa kana ghorofa moja pamoja na makorokocho kibao.
View attachment 1861941View attachment 1861942
Kaka hiyo ni kumtafuta fundi chuma mmoja akate na kuchomelea partition jinsi unavyotaka, aki reinforce hizo partiition na angle bar au square bar, then unaanza kupanga container zako kutokana na design unayohitaj,
ukiwa umeshaziwekea saddles ( nguzo za zege kushikilia hizo container.. ili kubalance centre of gravity na kuzi lock container kwenye hizo nguzo za zege isije upepo ukadondosha container la juu
baada ya kupanga na kukata bas tafuta fundi seremala mzuri mbao apige Marines boards zile nene ambazo zitakuwa kama kuta kwa ndan na nje pia chini na juu , baada ya hapo basi unatafuta mtu wa madirisha na milango anaweka kisha unamalizia na mtu wa wiring ya umeme plus mtu decor kwa ajili ya paints na finishing touches
kwa kifupi inakuwa ni nyumba ya bati na mbao.. kama nyumba za ulaya tu ambazo msingi zege ila kuta, ceiling na floor zote mbao, ndo maana wazungu ni rahs kuvunja nyumba ndan kuongeza upana wa sebule au jiko maana anatoa mbao anaweka. zingine. au akitaka mlango anatoboa mbao tu
ukitembelea warehouse nying za makampun ya hardware ujenzi au maviwanda ama haya makampuni ya nayofanya project kwenye remote locations mfano ujenzi wa barabara utaona makaz yao mengi ni containerized, kama kule moro kwenye bwana la nyerere, sema wao yanatengenezwa kutokana na mazingira husika..
hadi vyoo vinakuwa mobile wakihama kambi wanabeba tu .
ukitak ready made kutoka kwenye kampuni au kampuni ndo ikufanyie kazi hiyo utajikuta unalipia mara tatu ya gharama halisi..