Ni wapi nitapata mwanamke wa kuoa?

Haya uliyoyasema inawezekana yakawa yana ukweli kabisa, lakini napenda kukufahamisha ya kuwa hapo kwenye nyekundu ndie ninaye mtafuta, ili tuweze kuzoeana na kufikia yale malengo yetu. Hapa ungenisaidia ni wapi nitampata huyo amabye atimaye nimfanye awe rafiki yangu kwa muda kabla ya kuoana. Tatizo nililonalo ni kukosa ile social interaction, hili nalitambua kabisa, na haya yote yanasababishwa na shughuli zangu za kila siku. Natoka kwenda job alfajiri sana na ninarudi home jioni kati ya saa 11 na 12. Na nikirudi home nakua nimecho hivyo nalala (hii ni kutokana ya kwamba huwa situmii kilevi cha aina yoyote ile, so siwezi kwenda bar au sehemu yoyote ya kujumuika na jamii nyingine, pia sasa hivi siendi tena disco kama ilivyokua hapo awali hii ni kutokana na kuona nimecheza sana na sasa natakiwa kujenga maisha.
Mara nyingi nakua safarini nje ya dar, hivyo kunifanya kila wakati nakutana na watu wapya kwa muda fulani tu, tena hawa nifanyao kazi tayari ni watu wazima na pia wanafamilia, najikuta nina wakati mgumu sana.

Pia umezungumzia ukae na mtu kwa muda ukimchunguza, lakini nadhani hata ukienda kwa daktari atakuuliza maswali ya awali kabla ya kukutibia, mfano: umri, unaishi wapi, etc..... Sasa kwa mfano mimi binafsi nimejiwekea mke ninayemtaka atleast awe na umri wa kuanzia miaka kadhaa hadi kadhaa, sasa unakuta hata umrini mdogo sana hata hakaribii pale unapotaka au amezidi sana (ingawa mapenzi hayachagui umri, ila kila mtu na mtazamo wake katika kuchagua ili kutimiza matakwa yake) hapa pia napenda kusisitiza kama walivyosema wenzangu na mimi pia natambua ya kwamba hakuna binadamu aliyekamili, lakini atleast aguse pale unapotaka wewe. Ni hayo tu
 
hebu tuambie gud boy unataka mwanamke wa aina gani mwaga cv ya umtakae hapo nitakuagizia mahali
 
hebu tuambie gud boy unataka mwanamke wa aina gani mwaga cv ya umtakae hapo nitakuagizia mahali

Nashukuru sana kwa swali hili

1. Awe mchamungu
2. Awe na upendo kwa watu wote
3. Awe muwazi na mkweli
4. Awe na umri wa kuanzia miaka 25 hadi 28 (ila naweza kufikiria kubadilika ikiwa itakua ni tofauti kidogo na hapa)
5. Awe anafanya kazi (kujiajiri au kuajiriwa)
6. Elimu ya chuo
7. Ningependa zaidi akiwa anatokea mikoa ya pwani (Znz, Dar, Tanga, Morogoro, n.k hii pia inaweza kubadilika kulingana na atakayejitokeza)
8. Awe matured enough na kufikilia maendeleo ya familia yetu
9. Awe mzuri wa wastani, asiwe mnene, urefu wa wastani na mweupe ila sio wa mkorogo (natural color)
10. Asiwe aliwahi kuolewa au kutoa mimba
11. other added advantage
 
Kweli swali gumu ila mke unaweza kumpata popote kwenye
daladala
kanisani
kazini
mtaami
chuo
harusi
au sherehe yeyote
club
msibani
anywhere mkuu endelea kusearch hata humu jf[/QUOTE]


unamfagilia nani kwenye hii red?
 
 

hii cv mmmmhhhhh mpaka upate mwenye kufikia vigezo vyote hivi itabidi utafute sana,na wewe sifa zako ni zipi?
 
-sijakuelewa
 
Kamanda umeadimika kweli ndo mambo ya kusaka jiko nini?
Nakushauri ukamate Mwalimu wa shule ya Msingi au wa O'Level


usimdanganye mwenzako
ivo vgezo vilikuwa zaman..skuizi WENGI WAO wamechafuka..ni km wanawake wengne tu wa benk au maviwandani

anafanya wap aijalish we mchek km YALIYOMO YAMO BASI chukua..lakin kanuni ya naoa mwalimu au nes ahh ikimbie ao waliopata 4 afu wakafanya ualimu ni otenative ya maisha?wamevaa vimini weee wamecholka ndo wakaamua kwenda ualimu..?kaenda education cz kakosa coz ingne..ahh apana

pga got mungu atakupa sawasaawa na mapenz yako

pole brada
 
Kweli swali gumu ila mke unaweza kumpata popote kwenye

anywhere mkuu endelea kusearch hata humu jf
JF sikushauri maana kuna wadada wasioleweka hata kidogo mfano FF, Muonekano ni mzuri (avartar) anaweza kutoa point mpaka ukam-admire lakini siku nyingine anachemka kichizi mpaka unafikiria labda kuna kichaa kaiba password yake. Mwingine Rose1980 huyu naye aeleweki hata kidogo hivyo maeneo mengine sawa lakini JF NO.

Kwa kigezo cha sura nakushauri nenda Kituo cha Posta Mpya saa za jioni, uwezi kosa sample ya kama kumi hivi halafu endelea kuchambua kutokea hapo. Uzuri hawakatai kutoa namba za simu.
 
Umesahau bebii kuweka Bar vp tena jamani?

Hata kwenye lifts huko kwenye majengo marefu marefu nako awe anatembelea, ila hapa JF ndio mwisho wa yote atapata aliyefundwa haswa!
 
Kijana umesha pata huyo mke?
 
Pole isije ikawa unatafuta mke wa kufikirika ambaye ana macho ya AmIna, miguu ya Asha, Sura ya Bebii, kiuno cha Fatuma, nywele za Agnes, Mwanya wa Wema na Shingo ya Tausi na tabia ya Agel kwa pamoja ili awe mke wako. Ukweli ni kwamba hakuna mwanamke mwenye vigezo vyote hivyo tafuta tu yule mwenye minimum qualification. Mara nyingi sura na tabia zinakuwa negatively correlated, Hivyo Mtangulize Mungu kama upo serous atakusaidia. Wengine wanaweza kuwa wanafiki na wapole wakati wa uchumba lakini ukishamuoa anonyesha makucha yake.
 
Muombe sana mungu akupe mke mwema unayefanana naye, ila sio nawe uombe kupata mke mwema wakati mwenyewe unakuwa hujatulia, na ndio mana nikasema mke unayefanana naye
 
nimejaribu kuelezea kwa kila mchanganuo uliotoa

 
inamaana wewe hukua na uhusiano wa kimapenzi na msichana yyt yule ukitaka kupata mwenza best anza naye urafiki sio unakurupuka nataka nikuoe wengi wao wakisikia hiyo habari kama walikua na tabia chafu huzificha tabia zao lkn akishaingia kwenye ndoa utajuta.......makucha yote ya tabia mbaya utayaona kwahiyo anza naye urafiki mchunguze trtb ukiona anakufaa muoe
 
nina ushuuda kwa wanawake wa gongolamboto au pale kinondoni maeneo ya soko la TX ni wake bora..ni hayo tu kwa leo.
 
Kaimbe kwaya, nakupa wiki mbili tu, unapata wa kuoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…