Gudboy
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 867
- 82
- Thread starter
- #41
Haya uliyoyasema inawezekana yakawa yana ukweli kabisa, lakini napenda kukufahamisha ya kuwa hapo kwenye nyekundu ndie ninaye mtafuta, ili tuweze kuzoeana na kufikia yale malengo yetu. Hapa ungenisaidia ni wapi nitampata huyo amabye atimaye nimfanye awe rafiki yangu kwa muda kabla ya kuoana. Tatizo nililonalo ni kukosa ile social interaction, hili nalitambua kabisa, na haya yote yanasababishwa na shughuli zangu za kila siku. Natoka kwenda job alfajiri sana na ninarudi home jioni kati ya saa 11 na 12. Na nikirudi home nakua nimecho hivyo nalala (hii ni kutokana ya kwamba huwa situmii kilevi cha aina yoyote ile, so siwezi kwenda bar au sehemu yoyote ya kujumuika na jamii nyingine, pia sasa hivi siendi tena disco kama ilivyokua hapo awali hii ni kutokana na kuona nimecheza sana na sasa natakiwa kujenga maisha.mkuu inawezakena una udhaifu katika suala zima la kutafuta kitu unachohitaji , elewa kwamba
- kuna vitu unatakiwa wewe kama wewe uvione kwa mwenza unayemfikiria
- kuna mambo ambayo ni vigumu kuvipata kwa siku moja ila unatakiwa umweke karibu kwani jinsi anavyokuwa karibu anapoteza nguvu asili ya kuficha kitu
- wewe yawezekana una haraka sana ya kufikia malengo yako
- mfanye mtu unayetarajia kama rafiki yako wa karibu
- usiwe mwenye misimamo na imani zako zinavyokusukuma iwe na ndiyo iwe
Mara nyingi nakua safarini nje ya dar, hivyo kunifanya kila wakati nakutana na watu wapya kwa muda fulani tu, tena hawa nifanyao kazi tayari ni watu wazima na pia wanafamilia, najikuta nina wakati mgumu sana.
Pia umezungumzia ukae na mtu kwa muda ukimchunguza, lakini nadhani hata ukienda kwa daktari atakuuliza maswali ya awali kabla ya kukutibia, mfano: umri, unaishi wapi, etc..... Sasa kwa mfano mimi binafsi nimejiwekea mke ninayemtaka atleast awe na umri wa kuanzia miaka kadhaa hadi kadhaa, sasa unakuta hata umrini mdogo sana hata hakaribii pale unapotaka au amezidi sana (ingawa mapenzi hayachagui umri, ila kila mtu na mtazamo wake katika kuchagua ili kutimiza matakwa yake) hapa pia napenda kusisitiza kama walivyosema wenzangu na mimi pia natambua ya kwamba hakuna binadamu aliyekamili, lakini atleast aguse pale unapotaka wewe. Ni hayo tu