Mtoa mada naanza hivi, story yangu yakuhaso inaanza 2011 MMorogoro, baada ya kumaliza form 4 nilifeli, ilikuwa kipindi kigumu sana kwangu, form 4 nilimaliza 2010 ,ndio nilipoamua kwenda Morogoro kwa baba mdogo kusomea udereva katika chuo cha national sugar ilovo[Mkamba Kilombero].
Nilipofika tu nikaanza chuo nakumbuka nilisoma kwa miezi 3 hivi, nyuma ya nyumba ya baba mdogo kulikuwa na shamba nusu heka pembeni kulikuwa namfereji ambao unajaa maji full kila mvua inaponyesha, maji hayo ndo watu walikuwa wanatumia kunyeshea mashamba yao.
Kilombero ni sehemu iliyobarikiwa sana, kuna wakulima wa mpunga, miwa n.k, pia kuna wafugaji wa nguruwe, kuku n.k, lile shamba nilimuomba mwenyewe nililime akakubali maana lilikuwa kama pori hakuna aliyekuwa analima, jamaa alikubali nilime bure sikumpa ela yeyote.