Ni watanzania wangapi wanaofundisha soka nchi za nje ?

Ni watanzania wangapi wanaofundisha soka nchi za nje ?

Kwa kifupi ni hakuna.
Na sababu kuu nafikiri wengi wameridhika hapahapa nyumbani kwakuwa katika ukanda wetu wa EA sisi ndio tunaolipa vizuri zaidi kuanzia benchi la ufundi mpaka wachezaji.
Timu zetu zina uwezo wa kumsajili kocha na top player yoyote katika ukanda huu lakini majirani hawana msuli wa kumnyakua top player katika ligi yetu.
 
Wakafundishe wapi kwa short course zetu za wiki mbili mbili?
Burundi wametengeneza mfumo mzuri kufundisha makocha. Wanaenda Sana Belgium na France kwenye kozi za kuekeweka na muda wa kutosha. Sio hizi za wakufunzi was CAF waliojichokea.
Aiseeee
 
Mkuu kiufupi hatuna na tatizo ni lugha, lugha ya malkia inasimama kama limiting factor, nimekuwa nikijiuliza hili swali muda mrefi sana, nashukuru umeleta mawazo yaliyoshabihiana na yangu.

Kiufupi hakuna makocha wa kibongo nje!
Japo sisi tuna import sana hasa toka inchi jirani karibu zoote, kenya, uganda, rwanda, burundi, congo, zambia, malawi. Na mbaya zaidi ukienda ktk inchi hizo ni ngumu kukuta kocha mtanzania!!


TUNAKWAMA WAPI??
Rwanda na Burundi Kuna Kiingereza!?Mimi nafikiti kuna shida somewhere
 
Kwani huyu MWINYI wa yanga si mzanzibari alikua anafundisha huko congo sasa karudi? Asiwachanganye na mbwembwe zake za kuongea kama Werason ni Mtanzania fyoko yule wa mkunazini
 
Mimi nafundisha timu daraja la kwanza huku Turkey
 
Tunaambiwa Matola anatakiwa nje ya nchi .
 
Back
Top Bottom