Ni watu wa aina gani wanaofanya kazi Ikulu ya Marekani au Urusi??

Ni watu wa aina gani wanaofanya kazi Ikulu ya Marekani au Urusi??

Eti wakuu, leo wakati ninatazama Al Jazeera ghafla ikaja akili mwangu kujiuliza, hivi Ikulu za nchi kama Marekani, Russia, China au Uingereza kuna watu wa aina gani kule wanaajiriwa??

Kwa maana wale jamaa, habari za dunia nzima wanazo, brands zote kubwa duniani ni zao (Google, Microsoft, Meta).

Mambo yanayoendelea katika Ikulu za nchi zote duniani wanajua.

Kuna watu watabisha kuwa Google au Microsoft sio Mali ya Ikulu ya Marekani, but mind you uratibu wa shughuli zote za Marekani mpaka biashara na maisha ya mtu mmoja mmoja hufanyika state house.

State house ikiwa mbovu, tegemea nchi mbovu.

Ni kina nani wanafanya kazi Ikulu za Marekani, Russia na China??
Binadamu
 
Wabongo bana bora umewajibi eti wanaamin ni watu wanaakili sana kitu ambacho sio
Wewe unaona Kremlin au White House kuna vilaza kule. Wale wanajua mpaka ndani ya Ikulu zingine wanapanga nini duniani kote, sasa hao ni watu wa kawaida??
 
Duh!...hii kali...
Sera zote za nchi za kijamii mpaka kibiashara zinaanzia ofisi kuu ya Taifa na wao ndio wanaoweza kuzibadili, kubali au kataa.

Bila kuwa na sera bora sahau kuwa na taasisi kama Microsoft au Boeing
 
Eti wakuu, leo wakati ninatazama Al Jazeera ghafla ikaja akili mwangu kujiuliza, hivi Ikulu za nchi kama Marekani, Russia, China au Uingereza kuna watu wa aina gani kule wanaajiriwa??

Kwa maana wale jamaa, habari za dunia nzima wanazo, brands zote kubwa duniani ni zao (Google, Microsoft, Meta).

Mambo yanayoendelea katika Ikulu za nchi zote duniani wanajua.

Kuna watu watabisha kuwa Google au Microsoft sio Mali ya Ikulu ya Marekani, but mind you uratibu wa shughuli zote za Marekani mpaka biashara na maisha ya mtu mmoja mmoja hufanyika state house.

State house ikiwa mbovu, tegemea nchi mbovu.

Ni kina nani wanafanya kazi Ikulu za Marekani, Russia na China??
Hizo nchi hawaajiri binadamu wa kawaida wengi wao ni kutoka mars au multiverse universe
Mfano marekani inalindwa na Avengers
 
Hizo nchi hawaajiri binadamu wa kawaida wengi wao ni kutoka mars au multiverse universe
Mfano marekani inalindwa na Avengers
Kuna watu wanabisha humu mkuu. Wanadhani White House wanaingizana ingizana tu eti kwa kuwa ni mtoto wa DPP au RPC Mstaafu..
 
Ila wewe jamaa akili yako imejaa illusions sana. Hao ni watu wa kawaida sana tu, hata wewe unaweza kuajiriwa Ikulu. Kuhusu kupata taarifa hilo ni suala la mifumo ya usalama waliyonayo. Ukiwa na mfumo thabiti na imara basi utapata taarifa nyingi na sahihi, na mfumo wako ukiwa dhaifu basi kinyume chake
Anachojua hiyo mifumo ipo jengo jeupe 😄😄
 
Intel Test
Psycho test
Phizico Test
Bg Check up
Polygraph Test....
 
Hakuna mtu wa kawaida White House mkuu. Unataka kuniambia Marekani hawajui kinachoendelea Ikulu ya South Afrika au Brazil.

Kabla ya Rais wa North Korea kwenda Russia kwa ziara ya kikazi, Marekani alilisema hilo two weeks before.

White House labda kuna aliens mule wanafanya kazi aisee..
Umeuliza swali badala usubiri ujibiwe unajijibu mwenyewe! Taarifa za Korea ya Kaskazini Marekani anaweza kuzipata kupitia Korea ya Kusini kwa sababu ni washirika.
 
Umeuliza swali badala usubiri ujibiwe unajijibu mwenyewe! Taarifa za Korea ya Kaskazini Marekani anaweza kuzipata kupitia Korea ya Kusini kwa sababu ni washirika.
Korea Kusini ni Jimbo la Marekani, kama ilivyo Israel kule middle east..
 
Kweli tembea uone.
Mtu yupo mwatulole au mbagala anazungumzia mambo ya W. House, na bila aibu unasema wanaajiri watu gani.

Mkuu hao ni watu wa kawaida tu( huoni trump ni kichaa aliyeshika madaraka) hizo nchi zina ujinga mwingi sana sema tu huwezi kuyajua yote.

Ni kama vile mtu aliyeko huko china au japan akisikia Afrika anajua kila sehemu ni mapori na mistu.
 
Kwa upeo finyu wa mleta mada anadhani kuwa nujia ya kupatia habari ni Google na alizozitaja pekee.

Nendab kasome kuhusu "intelligence and information gathering in USA" làbda utapanuwa upeo wako.
 
Back
Top Bottom