Ni watu wachache sana wenye uwezo wa kusimama Taifa linapoenda sehemu isiyo sahihi

Ni watu wachache sana wenye uwezo wa kusimama Taifa linapoenda sehemu isiyo sahihi

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
796
Reaction score
2,028
Naandika makala hii fupi sio kwa nia mbaya hapana! Ila kuonesha sura ya taifa letu pendwa la Tanzania niko tayari kukosolewa au kusahihishwa sehemu yoyote ntakayokosea. Ukiangalia kwa makini sana utagundua ni watu wachache sana wenye uwezo wa kusimama pale taifa linapokosea au kwenda sehemu isiyo sahihi.

Kuna watu walionya juu ya mitaala yetu ya elimu kwa ngazi zote kuwa imepitwa na wakati hivyo ifumuliwe ili kukidhi mahitaji ya sasa lakini mpaka leo ni kitendawili ambacho mpaka leo hakijateguliwa matokeo yake wote tunaona graduates wanavyohenya mitaani hawajui watafanya nini?

Taifa la watu waoga linaharibika taratibu na madhara yake nimekubwa. Tuna jamii ambayo mtu anaogopa kwenda kwenye taasisi au ofisi ya umma kueleza shida yake, tuna jamii ambayo media house ziko biased na kusifu wanasiasa wakubwa ili kuvimbisha matumbo yao, tuna jamii ambayo watu wanajadili watu badala ya kuzungumza masuala na future ya taifa Mungu tusaidie.

Taifa la waoga linaumiza sana msomi tena professor anatoka jalalani ( chuo kikuu ) kisa amelamba uteuzi kuwa Waziri wa katiba na sheria za nchi yetu Mungu tusaidie. Kama tuna intellectual warriors wenzangu nisaidieni maana siwaoni naona wasaka fursa tu wakila na kuvimbewa

Ninayo mifano mingi tu ila naomba kuishia hapa ili wengine mchangie kuhusu taifa hili la waoga
 
Back
Top Bottom