Ni yapi maoni yako kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoripoti maafa ya kuanguka ghorofa Kariakoo?

Inasikitisha sana1
 
Najaribu kuwaza kwa sauti kubwa tena kwa kuweweseka tu: Mtu unaeneo lako kubwa tu umejenga mjengo wa ghorofa kadhaa na humo wanaishi ndugu zako wa karibu pamoja na wapangaji.
Mjengo unatitia asubuhi na mapema wakati umeishawasha VX lako kuanza safari kuelekea kanda ya kaskazini magharibi ambako una mwaliko wa mkutano unaowahusu wazito wa Dunia, wewe ni mwalikwa unayetarajiwa kutoa neno la shukurani...
Mjengo ulioanguka umeegemea upande mmoja zaidi ambapo kuna chumba cha watoto wako wa kiume na kifusi kilichoshuka kutoka ghorofa za juu, kimefunika kabisa eneo lote na hakuna taarifa za idadi ya walioko chini. Juhudi za uokozi zinasuasaua na hakuna kitengo kinachoaminika kutoa hata huduma ya kwanza...

Je! ..katika hali kama hiyo utaamua kuwasha gari lako mwenyewe uliloliandaa kwa safari kwenda kwenye mkutano ? Au utaomba udhuru na kuahirisha hiyo safari na kushughulika na maafa yaliyoikumba familia yako na jamii inayokuzunguka? 🤔😎
 
HII POST YAKO IMENIBARIKI SANA !!
NI POST MUHIMU SANA NA YA KIZALENDO.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Nashangaa sana nikiona kijana ni mwanachama wa ccm wao wanachoweza ni kuiba kura tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…