Kuna mambo basi tu umasikini na labda ubishi na ujinga.
Maana kuna sare za kuendeshea hivyo vyombo kuanzia kofia, glavu, koti, buti, viviko, magoti gadi. Nadhani yangefuatwa hayo yote ingewezekana kupunguza madhara.
Lakini jiulize bodaboda wangapi 'watajipamba' kikamilifu hivyo - Umasikini
Na wateja wangapi watakubali kupambwa hivyo? rejea kipindi kile suala la helmenti za abiria - Ubishi na Ujinga.
Hata hivyo kimsingi hivi vitu vyote vinabebana, kila mtu angemiliki walau ka gari kadogo bodaboda isingekuwa public transport. Kwanza cheki public gani ya wasafiri wawili wawili??
Kujibu swali kako ntasema hakuna kilichobadilika, adui zetu ni walewale wa tangu na tangu UMASIKINI, UJINGA NA MARADHI
Na ili tuendelee, tujikwamue hapo tutahitaji ARDHI, WATU, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA. Hakuna mchawi hapo