OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Nimemaliza kusoma andiko lililochapisha Review of African Political Economy likizungumzia Tanzania's Solidarity Tax, yaani kodi ya uzalendo ambayo ilianzishwa mwaka 2021 robo ya tatu.
Mtafiti katika andiko hilo ameweka sababu nyingi ya kuwa Tanzania haihitaji kuwa na tozo ya uzalendo, zifuatazo ni baadhi ya hoja alizoweka mtafiti.
1. Kodi ya Uzalendo huwa in muda wa kuisha
Kodi ya uzalendo huwa inaenda kwa muda fulani na huondolewa baada ya muda huo kuisha. Kodi hii inaweza kutozwa kwa muda wa mwaka au muda wowote uliokuwa allocated. Suala liko tofauti kwa Tanzania ambayo haijasema kodi hiyo itaisha lini.
2. Kodi hii hutumiwa wakati wa dharura
Nchi zote zilizotumia kodi hii zilifanya hivyo wakati wa dharura. Hata hivyo kwa Tanzania kodi hiyo ilitajwa kwenda kujenga madarasa na zahanati jambo ambalo linaweza kuwa plannned sio dharura. Dharura ingeweza kuwa COVID-19 lakini haiwezekani kwa kuwa wakati ule nchi ilipokea fedha za dharura kutoka IMF
3. Tanzania inapoteza fedha nyingi kwa mifumo hovyo ya kodi
Kila mwaka Tanzania hupoteza zaidi ya trillioni kutokana namifumo mibovu ya kodi, misamaha isiyo na tija na mambo mengine kama hayo. Mtafiti ameshauri kuiimarisha mifumo ya kodi ili kuweza kupata fedha yote ambayo kwa sasa inapotea. Kiuhalisia bado mapato mengi yanapotea ndio sababu ya kuwa na ratio ndogo ya kodi kwa GDP.
Kusoma andiko hilo bofya Tanzania’s solidarity tax