Ni zamu yako tunasemaje kwa kingereza" jifunze hapa

Ni zamu yako tunasemaje kwa kingereza" jifunze hapa

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Hili ni swali kutoka kwa mmoja wa wafuatiliaji wa ukurasa wetu kutoka mkoani Mara.

Ukitaka kusema ni zamu yako, huwa tunasema “It’s your turn…”.

Kuna baadhi huwa wanasema “It’s your duty….”. Hii sio sahihi, kwa muktadha wa zamu.

Wengi wanaosema “It’s your duty”, husema hivyo kwa kuwa shuleni tulizoea kumwita mwalimu wa zamu kama “T.O.D” ikiwa ni kifupi cha “Teacher On Duty”.

Ni kweli mwalimu wa zamu anafahamika kama “Teacher On Duty” kwa Kiingereza. Lakini inapokuja suala la kumaanisha zamu ya mtu kufanya kitu fulani, hatusemi “It’s your duty”.

Endapo utasema “It’s your duty”, utamaanisha “ni wajibu wako”. Inakuwa haina maana ya zamu tena.

TUTAZAME MIFANO ILI TUELEWE ZAIDI:

1. It’s your turn to wash the dishes today. (Ni zamu yako kuosha vyombo leo.)

2. It’s your turn to pay the bill. (Ni zamu yako kulipa bili).

3. It’s our turn to rest. (Ni zamu yetu kupumzika).

TUISHIE HAPA KWA WAKATI HUU.

POST HII NI MAALUMU KWA BEGINNERS. UNAPOANZA KUJIFUNZA LUGHA NI LAZIMA UJIFUNZE MANENO YATAKAYOKUSAIDIA

FB_IMG_17191278661954574.jpg


KUWASILIANA KATIKA MAZINGIRA YANAYOKUZUNGUKA.

KUSEMA NI 'ZAMU YAKO KUFANYA KITU FULANI', NI JAMBO LA KAWAIDA KATIKA MAZINGIRA YOTE. KUANZIA MAZINGIRA YA NYUMBANI HADI KAZINI
 
Vipi kama nitamwambia mwenzagu,
"Time ama a time to play your part" nitakuwa simaanishi zamu yako sasa..!?
Kabisa tunajifunza kupitia Kingereza cha waingereza sasa hawa wengine wa kina Marekani tuachane nao
 
Tatizo lako moja tu unakitafsiri kingereza kwa kiswahili. Hauko sahihi

Duty as Tax
The Duty on alcohol was raised soon after Magufuli died

Duty as task
As a father it's my Duty to take care of my family

Duty as Obligations or accountability
Teacher on Duty meaning it's the teacher obligation to teach.

Much respect nimependa huu uzi.
 
Back
Top Bottom