TIN ni Taxpayer Identification Number. Hii ni namba maalum ya mlipa kodi ambayo anasajiliwa kwa muktadha wa iwapo analipa kodi basi ndiyo inakuwa namba yake maalum ya uwasilishaji wa kodi.
VRN ni VAT Registration number. VAT ni kodi ya ongezeko la thamani ambayo mlaji anayotozwa na mfanyabiashara aliesajiliwa kwa mujibu wa sheria (VAT Act 2104) kwenye mauzo ya bidhaa na huduma zinazostahili kutozwa VAT. Namba maalum iliyosajiliwa kwa ajili ya kutoza na kuwasilisha hii kodi ya ongezekonla thamani ndiyo VRN.
Wanaostahili kusajili VAT kwa mujibu wa sheria ya ongezeko la kodi ya thamani ni pamoja na:-
1. Biashara yenye mauzo ya au yanayozidi mil 100 kwa mwaka
2. Watoaji huduma za kitaalam wanatakiwa kusajili VAT pasina kujali mauzo yao madogo au makubwa kiasi gani. Hii ina maana biashara yyt ya kitaalam km engineering, consultant, lawyer, wahasibu et al ni lazima kusajili VAT
3. Serikali na taasisi zake zinazofanya shughuli za kiuchumi za kujipatia kipato nje ya kazi zao za msingi hutakiwa kusajili
Nitasajili vipi VAT
1. Kuwa na namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN)
2. Kuwa na kiwango cha mauzo yanayostahili kutozwa VAT kwa mwaka kwa biashara
3. Kujaza fomu za maombi ya kusajiliwa kwa mujibu wa maelekezo
Faida za kusajiliwa VAT
1. Kuchangia pato la Taifa
2. Kiasi cha VAT kinachodaiwa na mfanyabiashara kinaweza kufidiwa na VAT kwa miezi inayofuata au mfanyabiashara ataomba kurejeshewa kwa kuzingatia marejesho ya kodi (Endapo VAT kwenye manunuzi ni kubwa kuliko kwenye mauzo)
(Sheria ya KODI YA VAT nimeambatanisha hapo chini waweza soma zaidi)
Nawasilisha
View attachment THE VALUE ADDED TAX ACT, 2014.pdf