Kwa mtazamo wako unahisi kunahaja ya kuendelea na huu utaratibu?
Wazazi wengi haswa vijijini wakiwaona binti zao wanakatiza mbele ya macho yao kinachowaijia kichwani kwa haraka ni mali.
Hii hupelekea mtoto wakike kuendelea kuwa mtumwa, picha linaanza anawekwa sokoni na mnaanza kupatana dau, toa kiasi hiki hapana icho sina labda nitoe hiki.
Akitoka hapo huyu mwanamke anakutana ndani na mume ambae kifikra anaona anamiliki kilakitu cha huyu mwanamke kwa sababu ametoa mali kumuoa.
Mtu mmoja anasema unatoa mahari kwa sababu watoto wataitwa kwa ubini wako. Huo ubini wangu unaweza kumpa mtu elimu, kazi, makazi na chakula Kama hauwezi kwann nitoe pesa kulipia ubini ambao hauwezi kumsaidia mtu kujikimu kimaisha?
Wanawake kama kweli mnahitaji usawa anzeni kwanza kuukataa huu utaratibu unaitwa mahari iyo ni biashara kama biashara nyingine.
Ni biashara kwa sababu inavigezo vyote vya kibiashara, Kipo kinachouzwa, yupo muuzaji, yupo mnunuaji, ipo fedha, yapo majadiliano ya iyo biashara, mashahidi n.k na ingependeza TRA waanze kukata kodi kwenye hii biashara