Ni zipi sababu za matumizi ya kokoto katika ujenzi wa reli?

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Habari za wakati huu wanajukwaa

Naomba mnitoe ushamba na mtujuze kwa wale ambao hatufaham ni sababu zipi za kiufundi hupelekea matumizi ya kokoto katika ujenzi wa njia za reli.

news18-26-6-167628080816x9.jpg
 
Zinawekwa ili kushikilia reli; kunyonya na kupupunguza mtetemo pamoja na kelele zitokanazo na msuguano kati ya reli yenyewe na magurudumu ya treni wakati treni ipitapo.
 
Safi kabisa mkuu, nadhani hiyo ni sababu mojawapo. Ipo sababu nyingine zaidi ya hiyo?
 
Nimefikiri na sijapata majibu sahihi, kama unafahamu sababu nieleze
Haya kwasababu umeomba na kuwa myenyekevu basi jibu lake ni hili:

Kokoto unazoziona kwenye reli zinajulikana kama "track ballast". Zinatumika kwa madhumuni kadhaa muhimu:

1. Utulivu: Ballast husaidia kuweka reli mahali pake, kuhakikisha inabaki sawa na imara wakati treni zinapopita.
2. Maji: Inaruhusu maji kutiririka mbali na reli, kuzuia mkusanyiko wa maji ambao unaweza kudhoofisha muundo wa reli.
3. Udhibiti wa Mimea: Ballast husaidia kuzuia ukuaji wa mimea karibu na reli, ambayo inaweza kuvuruga utulivu wa reli.
4. Usambazaji wa Mzigo: Inasaidia kusambaza mzigo kutoka kwa treni kwa usawa kwenye ardhi, kupunguza mkazo kwenye udongo wa chini.

Kwa kutumia mawe yenye ncha kali, ballast inabaki mahali pake na kutoa msaada unaohitajika na kubadilika kwa reli.
 
Mkuu, kwanza nilikuwa sifahamu kama inaitwa “ track ballast" Nashukuru kwa kunijuza.

Pia sababu ulizo eleza ni kweli zina mashiko na uhalisia, naamini wengi pia watajifunza kitu kwa hayo uliyo sema. Shukran sana Mkuu.
 
Treni ya SGR inatumia reli ya umeme hakuna kokoto. 😃😃
 
Back
Top Bottom