Ni zipi sababu za matumizi ya kokoto katika ujenzi wa reli?

Ni zipi sababu za matumizi ya kokoto katika ujenzi wa reli?

Ni hizo mbili tu. Kubwa zaidi ikiwa kupunguza kale ka-kelele ka vyuma kusuguana, gurudumu na reli.
Kwenye Kelele umepishana na ukweli Mkuu kidogo. Unapojenga Reli Mjini au Metro zinazopitia chini au juu ya Mji, huwa kuna Materials Kama kibao na yanakuwa yanabonyea kidogo Kama Mpira. Haya ndiyo hufungwa chini ya Reli na baadaye kwenye Mataluma na hupunguza makelele ingawa kwa kiasi kikubwa ni kupunguza Mitetemo inayotokea Train ikipita yaani Dynamic Force.
Kitu kikubwa kinachotumika kupunguza Makelele ya Kacha Kacha Kacha... ni kuziunga Reli kwa kuzichomelea pamoja.
Hata SGR wamechomelea wakati Reli ya Kati ni Kacha Kacha Kacha Kacha...
Mijini ambapo Reli na Magari yanapita pamoja, hakuna hizo Kokoto na mambo yanakwenda vema tu bila Kelele.
 

Attachments

  • A38-cheltenham-rd-northwards-montpelier.jpg
    A38-cheltenham-rd-northwards-montpelier.jpg
    1.1 MB · Views: 2
Back
Top Bottom