Ni zipi taratibu za kuanzisha NGO?

steveson manumbu

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
887
Reaction score
178
Wana Jamii forums kwa anae elewa taratibu za kuanzisha NGOs kwa Tanzania ambayo inafanya kazi nje ya nchi lakini wanahitaji kuwa na tawi kwa Tanzania,naomba kujuzwa taratibu zinazotakiwa kufuata ili kutambulika kisheria.

Asanteni.
 
Ni hivi mnaenda wizara ya maendeleo ya wanawake, jinsia na watoto. Kuna form watawapa mtajaza na kulipia dola kama 65 hivi na kupewa kitu kinaitwa COMPLIANCE CERTIFICATE. Hii inamaana kuwa mtakuwa mmeridhia sheria ya NGO YA 2002 ila mtaendelea kutumia katiba yenu na taratibu zenu nyingine ili mradi hamvunji sheria za nchi. Kila la kheri.
 
Habari zenu,pia nawapongeza sana katika moyo wenu wa kulijenga Taifa letu.
Mimi nauliza kuwa ukitaka kufungua NGO inakuwaje taratibu zipi zinafuata
 
kuna nyuzi nyingi humu zinazokuongoza ..hata mi nilipata kufungua yangu kwa kupitia moja kati ya nyuzi za huu..sijamaliza nimefika nusu. note that kuna ngo zaid ya 10000 zimefutwa mwaka jana kwahy wanabana sana kwenye kugawa vibali
 
Kama uko dar nenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto kitengo cha usajili wa NGO watakuelekeza. Kama upo mkoani kwa ufupi unatakiwa upitishe maombi yako kwenye halmashauri ya wilaya then mkoani. Baada ya hapo unaandika barua ya maombi ukiambatanisha na Katiba (nakala 3), majina ya waanzilishi na sahihi zao, muhtasari wa kikao cha kupitisha katiba, cv za watu watatu na passport size 2(Mwenyekiti, Katibu na Mtunza Hazina) pamoja na Form Na 1 iliyojazwa na kuwekwa stamp duty. Then utalipia usajii kutokana na ukubwa wa eneo inalohudumia NGO yako.
 
mkuu mawembesa kasema kweli . na jiandae kwa gharama mpya za usajili.
 
ingia online download how to start and manage NGO pdf book
 
habari zenu
nataka kuanzisha NGO, ninaomba mwenye kujua steps na costs zote jinsi ya kuanzisha, karibuni.
 
soma maelezo ya wadau hapo juu.ila vilevile sisi tulianzisha ya kwetu ila ndo mambo yakawa mengi ikatushinda kumanage.so tunatafta mtu wa kuinunua.tuna cheti na document zote muhimu na account kabisa.kama vipi nicheki 0717478451
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…